*Zaidi ya Sh 253 milioni kutumikaArusha.

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

Ulinzi wa Faru katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti na maeneo ya jirani,= unatarajiwa kuimarika zaidi baada ya kuanza mradi maalum wa Faru kufungwa vifaa vya technolojia za kisasa na hivyo kuwalinda na matishio ya ujangili ama kupotea.

Faru ni miongoni mwa wanyama ambao wapo hatarini, kutoweka duniani, kutokana naNkuwindwa na majangili, ambao wamekuwa wakiuza pembe zao na hivyo serikali imekuwa na mikakati kadhaa ya kuimarisha ulinzi wao.

Mwakilishi mkazi wa shirika la uhifadhi la kimataifa la Frankfurt zoological Society moja ya mashirika yanayoratibu mradi huo, Gerald Bigulube alisema mradi huo wa aina yake barani Afrika, unatarajiwa kuimalisha ulinzi na ufatiliaji wa faru katika eneo la Seregeti.

Alisema mradi huo unatarajiwa kutumia zaidi ya sh 253 milioni, zilizotolewa na shirika la uhifadhi la Friedkin Conservation Fund(FCF) na unaratibiwa pia na Shirika la hifadhi za Taifa(TANAPA) na Taasisi ya utafiti wa Wanyamapori(TAWIRI).

Bigulube alisema, tayari utekelezaji wa mradi huo, umeanza, ambapo mwaka jana faru 21 walifungwa vifaa maalum digital VHF na mwaka huu wengine watafungwa vifaa vya kisasa zaidi kutumia mfumo wa LoRa (LoRa System).

"lengo letu kama wahifadhi ni kuhakikisha Faru waliopo nchini wanaongezeka zaidi sambamba na wanyama wengine ambao maisha yao yamekuwa hatarini wakiwepo Tembo ambao nao tayari kuna miradi ya kuwafunga vifaa vya kisasa ili kuwafatilia "alisema.

Alisema katika kuhakikisha mradi huo unakuwa endelevu wameanza kuwapeleka kwenye mafunzo wahifadhi nchini Uholanzi ambao ndio watakuwa wakiratibu matumizi ya technolojia katika ulinzi na ufatiliaji wa faru.

"hivi karibuni tutaanza kuwafunga vifaa Faru, zoezi ambalo litatumia techolojia za hali ya juu,helkopta nna vifaa vingine vya kisasa kama ilivyokuwa mwaka jana"alisema.

Akizungumzia mradi huo, Mhifadhi Mkuu wa hifadhi za Taifa ya Serengeti, William Mwakilema alisema, mpango huo ambao unashirikisha wizara ya maliasili na utalii na wadau wengine utasaidia sana ulinzi wa Faru.

"Ulinzi wa Faru ni jambo ambalo ni nyeti na serikali na vyombo vyake imekuwa ikifatilia kwa makini hivyo,lengo kuu ni kuhakikisha wanahifadhiwa"alisema

Mtafiti kiongozi wa taasisi ya utafiti wa Wanyamapori(TAWIRI),Dk Edward Kohi, alisema ili kuimarishwa ulinzi wa faru, technolojia mbali mbali zinatakiwa kutumika.

"hii ni technolojia ya kuwafunga vifaa maalum, itawezesha kujulikana kila siku wapo wapi na hivyo ni rahisi kuwafatilia na kuwapa ulinzi"alisema

Tanzania ni miongoni mwa mataifa machache duniani, ambayo bado yana idadi kubwa wa faru ambao wamehifadhiwa katika hifadhi kadhaa za taifa, tofauti za nchini nyingine ambazo zimehifadhi Faru katika mashamba maalum
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: