Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya FINCA Microfinance, Nicholous John (katikati) akieleza waandishi wa habari kuhusu mikakati ya ushindani wa Kuza Ofisi na FINCA katika uzinduzi wa shindano hilo leo uliofanyika katika makao makuu ya Benki hiyo Jijini Dar es salaam. Kulia ni Afisa Mkuu Mtendaji wa Biashara wa Benki ya FINCA Microfinance, Emmanuel Mongella na kushoto ni Mtalaam wa Masoko wa Benki ya FINCA Microfinance, Noel Mulumba. Shindano la Kuza Ofisi na FINCA linalenga kuwapatia elimu ya biashara na fedha wamiliki wa biashara ndogo ndogo ambao baadae itapelekea katika kukuza biashara zao. Mshindi wa programu na shindano hili atawezeshwa kifedha kuendeleza biashara zake ndogo ndogo ziliyopo.
Afisa Mkuu Mtendaji wa Biashara wa Benki ya FINCA Microfinance, Emmanuel Mongella (katikati) akieleza waandishi wa habari kuhusu mikakati ya ushindani wa Kuza Ofisi na FINCA katika uzinduzi wa shindano hilo leo uliofanyika katika makao makuu ya Benki hiyo Jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya FINCA Microfinance bwana, Nicholous John na kushoto ni Mtalaam wa Masoko wa Benki ya FINCA Microfinance, Noel Mulumba. Shindano la 'Kuza Ofisi na FINCA’ kwa kuanzia litafanyika katika wilaya 4 za mkoa wa Dar es salaam, Kinondoni, Ilala, Temeke na Ubungo. Wilaya hizi zitaambatanishwa katika matawi ya benki yaliyoko Tegeta, Ilala, Victoria na kando ya barabara ya Pugu kuelekea Uwanja wa Ndege.
Afisa Mkuu Mtendaji wa Biashara wa Benki ya FINCA Microfinance, mmanuel Mongella (katikati) akieleza waandishi wa habari kuhusu mikakati ya ushindani wa Kuza Ofisi na FINCA katika uzinduzi wa shindano hilo leo uliofanyika katika makao makuu ya Benki hiyo Jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya FINCA Microfinance bwana, Nicholous John na kushoto ni Mtalaam wa Masoko wa Benki ya FINCA Microfinance, Noel Mulumba. Shindano la 'Kuza Ofisi na FINCA’ kwa kuanzia litafanyika katika wilaya 4 za mkoa wa Dar es salaam, Kinondoni, Ilala, Temeke na Ubungo. Wilaya hizi zitaambatanishwa katika matawi ya benki yaliyoko Tegeta, Ilala, Victoria na kando ya barabara ya Pugu kuelekea Uwanja wa Ndege.

·Shindano la miezi mitatu lina lengo la kutoa elimu ya fedha na biashara kwa wamiliki wa biashara ndogo ndogo.

.Benki ya FINCA Microfinance inaendelea kuwa benki ambayo inahamasisha ushirikishwaji wa kifedha katika kipindi cha miaka 20 na zaidi ya uwepo wake nchini Tanzania.

Benki inayokua kwa kasi zaidi nchini Tanzania, Benki ya FINCA Microfinance leo imetangaza uzinduzi wa programu ya miezi mitatu na shindano ambalo linalengo la kuwaongezea uwezo wajasiriamali wadogo kwa kuwapatia stadi za biashara, ufahamu na kisha kuwapatia zaidi ya TZS Millioni 10 kwa wazo bora la biashara litakalokuwa limewasilishwa.

Shindano linalojulikana kama 'Kuza Ofisi na FINCA’ kwa kuanzia litafanyika katika wilaya 4 za mkoa wa Dar es salaam, Kinondoni, Ilala, Temeke na Ubungo. Wilaya hizi zitaambatanishwa katika matawi ya benki yaliyoko Tegeta, Ilala, Victoria na kando ya barabara ya Pugu kuelekea Uwanja wa Ndege.

Akiongea wakati wa uzinduzi jijini Dar es salaam, Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya FINCA Microfinance bwana, Nicholous John alisema kwamba lengo ni kuwapatia elimu ya biashara na fedha wamiliki wa biashara ndogo ndogo ambao baadae itapelekea katika kukuza biashara zao, Mshindi wa programu na shindano hili atawezeshwa kifedha kuendeleza biashara zake ndogo ndogo ziliyopo.

"Shindano hili litashirikisha wateja wa FINCA wenye akaunti na wale ambao wanapenda kushiriki watatakiwa kufungua akaunti ya FINCA, ambao pia watatakiwa kuweka kiasi cha TZS 20,000 (Salio jipya katika akaunti zao) Watatakiwa kujaza fomu katika matawi ya FINCA ambapo watabainisha katika fomu hizo kuwa wataenda kufanyia nini zawadi hiyo katika biashara zao iwapo wataibuka kuwa washindi. Baada ya hapo fomu hizo zitawasilishwa katika matawi yetu, mpaka hapo watakuwa wametimiza vigezo vya hatua ya kwanza ya shindano".
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: