Baadhi ya watoto wakiwa kwenye foleni ya kupata huduma ya upimaji macho katika banda la Hospitali ya Taaluma na Tiba, MAMC wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika duniani katika viwanja vya TANESCO, Kinyerezi.
 Dkt. Nicholaus Benedicto akiwa anampatia huduma ya kipimo cha miwani kwa mtoto aliyetembelea banda la Hospitali ya MAMC wakati ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika Duniani katika viwanja vyaTANESCO, Kinyerezi.
 Dkt. Ally Omari akimgagua mtoto kujua tatizo gani la macho linamsumbua baada ya kusikiliza maelezo kutoka kwa mama yake wakati ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika Duniani katika viwanja vya TANESCO, Kinyerezi.
 Dkt. Edwin Greyson akifanya kipimo cha fundoscopia (kuangalia pazia la macho kama linaona vizuri kwa mtoto aliyejitokeza kushiriki wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika Duniani katika viwanja vya TANESCO, Kinyerezi.

Dkt. Nicholaus Benedicto akimuelekeza mtoto aliyepata huduma ya macho katika banda la Hospitali ya MAMC jinsi ya kuweka dawa kwenye macho wakati ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika Duniani 


Picha ya pamoja.Na Mwandishi Wetu.


Madaktari wa Macho walioshiriki katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika katika kutoa huduma ya upimaji wa macho katika viwanja vya TANESCO, KinyereziIdara ya Macho ya Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili -MAMC, Mloganzila wametoa huduma ya upimaji macho katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Africa yaliyofanyika katika viwanja vya TANESCO, Kinyerezi kuanzia tarehe 12 mpaka 14 mei 2018.


Akiongea katika maadhimisho ya siku hiyo Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, MUHAS na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Macho, Dkt. John Kisimbi amesema kuwa katika maonesho haya, Idara ya Macho imeazimia kutoa elimu kwa wazazi na watoto hususani kwenye magonjwa ya macho. "Vile vile, kwa kupitia zoezi hili la upimaji macho wanafunzi wetu wanajifunza mambo mbalimbali na pia tunapata nafasi ya kutangaza huduma mbalimbali zinazotolewa katika hospitali ya MAMC, Mloganzila,” Dkt. Kisimbi aliongeza.Mbali na kutoa elimu kwa magonjwa mbalimbali ya macho, Dkt. Kisimbi amesema katika maadhimisho haya Idara inatoa huduma ya kupima uwezo wa kuona, kujua hali ya jicho kwa ujumla kama ni zima au linauma, vipimo vya miwani hasa kwa watoto waliokuwa na uhitaji wa miwani pamoja na huduma ya dawa kwa watoto waliokuwa hawana shida kubwa ya macho na pia kutoa ushauri wa kwenda Hospitali kwa watoto wenye matatizo makubwa ya macho kwa ajili ya uchunguzi wa kina na matibabu.

Katika maadhimisho haya Siku ya Mtoto wa Afrika zaidi ya watoto mia mbili (200) waliweza kupata huduma ya upimaji wa macho kutoka Idara cha Macho ya Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi, Muhimbili (MAMC). 
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: