Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro akiwa na baadhi ya wananchi na abiria waliokuwa safarini wakisaidiana kuokoa majeruhi kutoka kwenye roli aina ya Scania lenye namba T 396 CCY iliyokuwa ikitokea Morogoro kuelekea Dar es salaam baada ya kupata ajali na kuanguka katika eneo la Bwawani mkoani Morogoro na kusababisha majeruhi mmoja ambaye ni dereva wa roli hilo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro (wa Pili kulia), akiwa na dereva wa roli aina ya Scania (wa pili kushoto) aliyeokolewa muda mfupi uliopita kutoka kwenye roli alilokuwa akiliendesha baada ya kupata ajali na kuanguka katika eneo la Bwawani mkoani Morogoro na kusababisha majeruhi mmoja ambaye ni dereva wa roli hilo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akisalimiana na kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma SACP Gilles Muroto, muda mfupi baada ya kuwasili mkoani humo kwa ziara ya kikazi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro (katikati), akizungumza na kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma SACP Gilles Muroto na kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Mugabo Wekwe alipokutananao katika mpaka unaotenganisha mkoa wa Morogoro na Dodoma kabla ya kuwasili mkoani Dodoma kwa ziara ya kikazi. Picha na Jeshi la Polisi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: