Meya Mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni Yusuph Mwenda (kulia) akiwagawia wageni zawadi.
MEYA Mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni Yusuph Mwenda na mkewe wakiwagawia wageni zawadi.
MEYA Mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni Yusuph Mwenda ameiasa Jamii kuendelea kudumisha amani na upendo katika jamii hususani kipindi hiki ambacho Taifa linapopiga hatua za kimaendeleo chini ya Uongozi wa Rais John Magufuli.

Mwenda aliyasema hayo jijini Dar es Salaam mara baada ya hafla ya Chakula, alichokiandaa maalumu kwa ajili ya watoto wanaoishi katika Mazingira magumu wanaolelewa katika kituo cha Malaika.

Alisema katika kipindi hiki ambacho Tanzania inaendelea 'kujengwa' kiuchumi kupitia miradi mbalimbali ya kimaendeleo, kuna kila sababu kwa wananchi wote kudumisha amani iliyopo nchini, kama hatua ya kuungana mkono maendeleo hayo.

Alisema katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Serikali ya awamu ya tano, Taifa limeshuhudia likitekeleza miradi mikubwa ya kimaendeleo, ikiwemo ya ujenzi wa miradi ya Reli ya kisasa(Standard Gauge),Bwawa la kuzalisha umeme la Mto Rufiji(Stiggler's George) pamoja na kuiunganisha mikoa mbalimbali kwa Barabara za lami.

“Sote tunashuhudia namna mbavyo Taifa letu linazidi kupiga hatua kuelekea mikakati ya Serikali ya ujenzi wa Uchumi wa Viwanda ifikapo 2025, ambayo kimsingi kama watanzania tunapaswa kuipongeza,lakini ili hayo yafanyike kwa ufasaha tunapaswa kwanza kudumisha amani yetu tuliyonayo” alisema Mwenda.

Aidha Mwenda katika hafla hiyo aliiomba jamii kuwa na upendo kwa watoto wadogo hususani yataima na wale wanaoishi katika mazingira magumu ili waweze kujiona kuwa sehemu ya familia zingine ambazo hazipo katika maisha wanayoyapitia.

Alisema watoto hao ambao wengi wao wamepoteza wazazi wao wana kila sababu ya kuonyeshwa upendo ili kuwajenga kisaikolojia wakati wote wanapokuwa katika maeneo wanayoelelewa ili kuwapa nguvu ya kuwafikisha katika malengo yao mbalimbali ya kimaisha.

“Tuwapende ili wajione na wao ni sehemu ya jamii nyingine tunazoishi sisi na familia zetu, kufanya hivyo kutawafanya wajisikie vizuri kama ambavyo watoto wengine waliopo katika maisha chini ya wazazi wao” alisema Mwenda.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: