Brother uyapokee yote nitakayokwambia, hata kama hutayapenda jaribu kuyaelewa kaka.

Nyakati nzuri na tamu zinazidi kupotea na wanaume bora na watundu wa mawazo na vitendo tunazidi kupotea. Tunazidi kuwa na idadi kubwa ya wanaume wadhaifu, wanaolalamika na wanyonge wenye mbwembwe na sifa zisizo zao.

Dear brothers ukiachwa na mwanamke haina haja ya kutengeneza kauli mbiu za hakuna wanawake bora siku hizi wala hakuna mapenzi ya dhati na kwenye social media sio sehemu sahihi ya kueneza maneno ya kulaumu wanawake unapoachwa.

Dear Brothers kama wanawake wanakusumbua kwenye mauhusiano, ni muda muafaka wa kujitenga na kujitathmini juu ya wanawake na ni muda wa kuwekeza kwenye mianya ya kutafuta pesa.

Ukiachwa, Kubali kuwa umeachwa kwa sababu zake mwenyewe mwanamke na tafuta mbinu nzuri ya kutibu moyo wako. Epukana kulalamika kila uchwao kuwa wanawake hawana mapenzi ya dhati.

Tatizo letu sisi vijana wa kiume, tunapenda sana mipira iliyokufa, mitelemko yaani finished products, tunawapenda wanawake wazuri, warembo, wenye swaga ila hatujui huo urembo umetunzwaje. Wapo wanawake ambao ni low profile, wanakabiliana na kila aina ya mazingira, ila hao hua tunawaona ni washamba.

Kuwa mwanaume kwa ubongo na kwa moyo kuweza kabiliana na changamoto za maisha na moja ya kigezo kikubwa cha kuwa mwanaume ni kuwa na kifua cha kutunza siri, kutokulalamika na ubongo wa kutafutia pesa.

Wanawake bora na watamu wapo wengi kila mahala ila wanapatikana kwa njia ya sala na maombi sababu hakuna mwanadamu aliyemuomba Mungu ampe mke mwema akapata majonzi na simanzi kwenye ndoa yake, ndoa huanza na Mungu na huiasha na Mungu.

Muombe Mungu akupe mke mwema na sio kutafuta demu bora kwa jicho lako na akili yako badala ya kuomba mke mwema kwa Mungu. Na ukiachwa na slay queen, kubali yaishe. Slay queen atabaki kuwa slay queen, wala hagusi kabisa level ya wife material. Acha kulalamika, Man Up my Brother!!!!

#KwaWanaumeWote

Imeandikwa na Mwijaku.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: