Mitandao ya Simu Tanzania nahisi ipo kwa ajili ya kutaka kuharibu Saumu za watu

Mnafanya Saumu yangu Ining'inie... MA ME MI MO MU zenu

Vodacom Tanzania, Tigo Tanzania , Airtel Tanzania , Halotel Tanzania inamaana hawa watu Hamuwajuiii...? au line si zenu hizi...?

Nyinyi ndo mnasema tuwe makini na Matapeli halafu leo hii matapeli hao hao mnawaona na hamfanyi jambo lolote hili ni jambo la kushangaza sana.

Kila kukicha matangazo ya waganga, matapeli wakijifanya wanakudai utupe pesa hivi kweli tunaelekea wapi??? Naowaomba wandugu mwenye kumjua hata mmoja tuwaumbue ili waache tabia hizi.

Kibaya zaidi na chakushangaza mitandao hii wanapokwenda Polisi kusaka wale wanatoa lugha za matusi kwenye mitandao ya simu wala wanakuwa mstari wa mbele kuwapatia maongezi mpaka meseji ya mwisho kuchat, ila jumbe za hawa matapeli mnajifanya hamzioni.

Au ninyi hamna line kama zetu ya kwamba hazipokei SMS hizi eti???.

TCRA nao sijui wako wapi jamani Mimiiiiiiiiii.

Naombeni Wanzanzania tupaze sauti ili kuweza kuondoa wimbi ili la utapeli lililotapakaa kila konaya nchi yetu, watu wachache wanachafua nchi.

Imeandikwa na 
Byego Sauti
===

VODACOM mtandao wenu umekua kero sana kwa sisi watumiaji hatujui ni kuna ushirikiank au mmekua rahisi sana kusajili.line za wezi, na kwa nn MSG za matapeli zinakuja kwa line ga VODA tu?

Mesaji za ile hela tuma hapa, zimekua too much, imagine nimesajili no.ty hata sijaitumia nikatumiwa msg za WAGANGA na za ILE HELA TUMA HAPA

Tutaanza ku-Tag Mawaziri husika kwenye kurasa zenu

Mary Joseph Waambie wajue mna siri gani na matapelii au lenu moja tunataka mkomeshe hizi meseji

Saraphina Timotheo wengine wanatupigia wakijidai wafanyakazi wenu wakitaka tuwatajie kiasi kilichopo kwenye akaunti zetu na namba za siri

Agnes Kimweri Kero kero kero kubwa na moja ya sms za kitapeli zinazotumwa ni hii:
IlE ELAITUME KWENYE NAMBA HII 0752161345 JINA LITAKUJA LAITON MTAFYA ILE NAMBA USITUMIE. FANYA HALAKA

Nyingine hii: SASA HIYO HELA NITUMIE KWENYE HII NAMBA 0746 562 155 SASA HIVI NATUMIA SIM YA WAKALA Jina Litatokea Fadhili Mbisa. Namba Yangu Imefungwa M Pesa Halafu Imezima Chaji.

Saraphina Timotheo ni kwamba hamuoni, hamjui au tuwaeleweje tunalizwa kila siku mkipigiwa oh! hela ishatolewa mbona vitu vngine mpo fasta hili vp?

Agnes Kangu Jana nimepigiwa simu kabsa eti nimeshinda pesa sijui tujue account yako ya M-PESA ina kiasi gani mfyuuuu... tumechoka.

Seychelela Peter Msamba Usumbufu wa VODA NI MWINGI SANAAAA BILA.WATEJA KUUUNGANA NA KUKEMEA TUTAENDELEA KUTAPELIWA

Saraphina Timotheo 0765009033 hiyo kanipigia nimeshinda laki 4 kutoka VODA nitaje kiasi nilichonacho kwa akaunti yangu.

Aishwarya Mohammed Kweli kabisa halafu huu ukimya wenu hatuuelewi tunaomba mtupe mwongozo maana tumechokaaaaaa.

Tausi Mgawe Mi hata lain ya voda nishaitupa maana it's too much to handle.

Habiba Issa Makota Voda mje msisome kimya kimya tumewachokaaa mnafuga wezi wa mitandao na matapeliii.

Mammy Ake Edith Edith JIUNGE FREEMASON Utajilike Kiuchumi Kibiashara Kidini Kisiasa Sanaa nk mpigie wakala wetu {n366tz} kwa hatua ya kwanza sim 0758325164 huduma inafika ulipo.

Mammy Ake Edith Edith BABU MIAMBI, Mganga wa tiba asili. Nyota, kumvuta mme/mke, nguvu za kiume, pete, biashara, jini mali, mali iliyopotea. 0742471110. ITAFIKA POPOTE.

Anny Kimario Halafu kama wanajua vile ukimaliza kuongelea swala la kutumiana pesa unaona na meseji ya ingiza kwenye hii no nipo kwa wakala fanya haraka. 

Usajili wa no sasahivi umekuwa wa kiholela. Hamfatilii mpo kimya tu. Hii tabia imekithiri mnooo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: