TAHARUKI kubwa imeibuka katika Mtaa wa Livingstone na Agrey Kariakoo jijini Dar es Salaam baada ya moto mkubwa kuzuka na kuteketeza ghala la kuhifadhi bidhaa mbalimbali lililopo mtaa huo.

Moto huo ambao ulisababisha moshi mkubwa kutanda angani na kuzua hofu kubwa kwa wamiliki wa maduka ulianza kuwaka mapema leo.

Hali ya kuwaka moto huo kwa kasi ulisababisha biashara katika maeneo hayo kusimama kwa muda kutokana na mkusanyiko wa watu waliokuwa wamefika kushuhudia.
Wakizungumzia tukio la kuwaka kwa moto huo baadhi ya wananchi wamesema kuwa walishuhudia wakiona moto mkubwa ukiwaka katika ghala hilo na hofu yao kubwa ilikuwa huenda ukaunguza na maghala na maduka mengine yaliyopo karibu na ghala lililokuwa linawaka.

Wamesema moto huo uliokuwa umeambatana na moshi mkubwa angani ambapo baadhi ya waliokuwa maeneo hayo ulisababisha baadhi ya watu kukimbia maeneo hayo.
Akizungumza moto huo, mmoja ya maofisa wa Jeshi la Zima Moto amesema wamefanikiwa kuzima moto huo na cha msingi waliudhibiti kwa kuhakikisha hauendi kuunguza maeneo mengine.

Moto huo ulifanikiwa kuzimwa mchana na ndipo baadhi ya wafanyabishara walipoanza kufungua maduka yao baada ya hali kuwa shwari.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: