Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipojumuika na Viongozi na Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi katika Futari aliyowaandalia jana katika Viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar ikiwa ni mwendelezo wake wa kufutarisha kila ifikapo kipindi kama hichi, (kulia) Rais mstaafu wa Zanzibar Dkt.Amani Abeid Karume
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein (katikati) akijumuika na Viongozi Wanawake na Wananchi wengine katika Futari aliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,katika Viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar jana
Baadhi ya Akinamama wa Mkoa wa Mjini Magharibi wakiwa katika Futari iliyoandaliwa jana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein katika Viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar katika mwendelezo wake wa kuwafutarisha Wananchi hao kila ifikapo Mwezi 27 wa Mfungo wa Ramadhan
Wananchi na Waislamu wa Mkoa wa Mjini Magharibi wakiwa katika Futari iliyoandaliwa jana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein katika Viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar ikiwa ni mwendeleo wake kila ifikapo mwezi 2y ya Mfungo wa Ramadhan kuwafutarisha Wananchi
Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji (kulia) alipokuwa akisoma Dua kumuombea Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) baada ya futari aliyoiandaa kwa Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi jana katika Viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar, ikiwa ni mwendelezo wake wa kuwafutarisha Wananchi na Waislamu wa Mikoa huo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akiagana na Wananchi mbali mbali waliohudhuria katika Futari iliyowaandalia Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi jana katika Viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar ikiwa ni katika mpangilio wake wa kuwafutarisha Wananchi na Waislamu wa Mikoa huo kila ifikapo mwezi 27 ya Mfungo wa Ramadhan.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: