Katibu wa Rais Ngusa Samike akimkabidhi Rehema Kadogosa ambaye ni Mama wa Mtoto Latifa Kadogosa (13) aliyelala kitandani kiasi cha Shilingi milioni tano (5,000,000/-) fedha zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya kumsaidia mtoto huyo ambaye ana matatizo ya kiafya jijini Dar es Salaam.
 Katibu wa Rais Ngusa Samike akimuangalia mtoto huyo Latifa Kadogosa(13) ambaye amepakatwa na Mama yake Rehema Kadogosa Mwenge jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Tawi la Benki ya CRDB Mikocheni Rehema Moyo akimkabidhi Kadi ya Benki Rehema Kadogosa mama mzazi wa Latifa Kadogosa mara baada ya kufungua Akaunti katika tawi hilo kwa ajili ya kutunza fedha hizo alizopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na fedha nyingine atakazosaidiwa na wadau wengine. PICHA NA IKULU.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: