Michuano ya Kombe la Sportpesa sasa imeweza kunoga baada ya Timu ya Singida United kutinga nusu fainali baada Simba SC iliyofuzu hatua hiyo jana.

Timu hizo mbili sasa zitakutana na timu za Kenya zilizofuzu hatua hiyo ambazo ni Gor Mahia na Kakamega

Homeboys huku Yanga na JKU (Tanzania) na Kariobangi na AFC (Kenya), zikiwa zimeshaaga mashindano hayo.

Singida United imefuzu hatua hiyo baada ya kuilaza AFC Leopard ya nchini Kenya kwa mikwaju ya penati 4-2 baada ya dakika 90 za mchezo kumalizika bila timu hizo kufungana.

Wapigaji wa penati hizo kutoka Singida walikuwa Keny Ally Mwambungu, Miraji Adam, Dany Lyanga, Sumbi Elinyesia na Shafiq Batambuzi, wachezaji wa AFC Leopard walikuwa Kambura, Wkooya na Isuza.

Michuano hiyo Sportpesa itatimua vumbi tena kwa timu zilizotinga nusu fainali kukutana Alhamisi ambapo Simba atachuana na Kakamega Homeboys huku Singida ikikutana na Gor Mahia
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: