Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai aongoza Waheshimiwa Wabunge katika kuuaga mwili wa Ndg. Mtuka Daniel Nguluba ambaye ni Baba Mzazi wa Mbunge wa Manyoni Mashariki, Mhe. Daniel Mtuka katika tukio lililofanyika leo tarehe 12 Juni, 2018 katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma.
Baadhi ya Waheshimiwa Wabunge wakibeba mwili wa Baba mzazi wa Mbunge wa Manyoni Mashariki, Mhe. Daniel Mtuka aliefariki juzi tarehe 10 Juni, 2018 katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma. Mwili huo uliagwa leo katika hospital hiyo Jijini Dodoma
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akimfariji Mbunge wa Manyoni Mashariki, Mhe. Daniel Mtuka baada ya kuondokewa na Baba yake mzazi aliefariki juzi tarehe 10 Juni, 2018 katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma.
Baadhi ya Waheshimiwa Wabunge, ndugu, jamaa na marafiki waliofika katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma kabla ya kuuaga mwili wa Baba mzazi wa Mbunge wa Manyoni Mashariki, Mhe. Daniel Mtuka katika tukio lililofanyika leo tarehe 12 Juni, 2018 katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma.
Spika wa Bunge, Job Ndugai (wa tatu kulia mbele), katibu wa Bunge, Ndg. Stephen kagaigai (kulia mbele) wakiwa pamoja na Waheshimiwa Wabunge, ndugu, jamaa na marafiki kabla ya kuuaga mwili wa Baba mzazi wa Mbunge wa Manyoni Mashariki, Mhe. Daniel Mtuka aliefariki juzi tarehe 10 Juni, 2018 katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma. ​ (PICHA NA OFISI YA BUNGE).
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: