Habari tulizozipata Globu ya Jamii hivi punde kutoka mkoani Kigoma mapema leo asubuhi hii ya Jumatano Juni 6,2018, inaelezwa kuwa Basi la Hamida Trans lenye namba za usajili T 885 DLD lililokuwa likitoka Kigoma kwenda wilaya ya Nzega mkoani Tabora limegonga treni ya mizigo (Garimoshi la mizigo) katika eneo la Gungu Mjini Kigoma.

Ripota Editha Karlo aliyekuwepo eneo la tukio na kushuhudia mandhari halisi ya jali hiyo,ameeleza kuwa ajali hiyo imetokea leo alfajiri, na mpaka sasa kwa taarifa za awali inaelezwa kuwa Watu 11 wanahofiwa kupoteza maisha,huku idadi ya majeruhi ikidaiwa kuwa ni 26.

Ripota wetu yupo eneo la tukio, hivyo tutaendelea kuwaleta habari kadiri ya zitakavyokuwa zikiingia.
Baadhi ya vyombo vya Ulinzi na Usalama wakiwa eneo la tukio la ajali.
Baadhi ya Askari wa JWTZ wakiwa tayari wamefika eneo la tukio kwa ajili ya kutoa msaada kwa namna moja ama nyingine.
Baadhi ya Wananchi waliofika kushuhudia tukio la ajali hiyo wakishuhudia majeruhi wakipakizwa kwenye gari ya Wagonjwa ya JWTZ tayari kupewa huduma ya kwanza na baadae kupelekwa hospitali kwa matibabu zaidi
Mbunge wa Kigoma mjini Mhe.Zitto Kabwe akiwa eneo la tukio la ajali akishuhudia majeruhi wakiokolewa.
Baadhi ya majeruhi wa ajali wakiendelea na matibabu katika hospitali ya mkoa wa kigoma.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: