Na Agness Francis ,Globu ya Jamii.

Halmashauri ya manispaa ya ubungo imewataka wakurugenzi kuwasimamisha kazi mameneja na wasimamizi wa masoko kwa ubadhilifu wa fedha za serikali.

tamko hilo limetolewa kwa ajili ya kupisha uchunguzi wa wizi wa fedha hizo.

Akizungumza na vyombo vya habari leo ofisini kwake Jijini Dar es Salaam Mstahiki meya wa halmashauri ya ubungo Boniphas Jacob amesema kuwa watumishi hao walikuwa wakikiuka sheria kwa kutopeleka fedha benki zinazokusanywa kupitia masoko hayo kama inavyotakiwa badala yake wanakaanazo wenyewe kwa lengo la kuziiba.

"Taarifa ya awali ilionyesha Kiasi cha Tsh 716 Millioni ndizo zilizokusanywa kwa Miezi 9, wakati taarifa sahihi baada ya ukaguzi wa Mfumo ni kiasi cha bilioni 1.009 ndizo zikizokusanywa kwa miezi 9,Hivyo kubainika kwa utofauti wa kiasi cha 273,131,441,00 ambazo zilikuwa azijulikani zilipo"amesema Meya Jacob.

Aidha amesema kuwa baada ya ukaguzi uliofanyika kuanzia tarehe 17 hadi 25 mwezi wa 4 mwaka huu waligundua kuwa kuna ubadhilifu umefanyika.

Ambapo baada ya kugunduliwa wamefanya utapeli wa kuiba ndipo walipoanza kurudisha kiasi shilingi mpaka kufikia shilingi milioni 131.

Miongo mwa watumishi hao ni meneja Obote Etta (mabibo ndizi), Greyson Sebastian (Simu 2000), Frida Michael (shekilango),Edwin Magita (mabibo), John Twakinde (mabibo),Bakari Mshonga (sinza2).

Sambamba na watumishi wengine ambao ni muweka hazina,afisa mapato pamoja na msimamizi wa mfumo wa manispaa hiyo ya Ubungo

Mjumbe wa kamati ya fedha halmashauri ya manispaa ya ubungo Liberata Samsoni amesema kuwa kitendo kilichofanywa na watumishi hao ni kuirudisha nyuma halmashauri na miradi ya maendeleo kama vile kujenga soko la kisasa.

Vile vile mwenyekiti wa maadili halmashauri ya manispaa ya ubungo Humphrey Sambo amesema kuwa ili kuhakikisha jambo lisijirudie tena walohusika na wizi huo wachukuliwe wafanyiwe uchunguzi na waliobainika wachukuliwe hatua za kisheria.

Sambo amemalizia kwa kuwataka wahusika wa kitengo cha ukusanyaji fedha za halmashauri wawajibike kusimamia vizuri na ikiwezekana mapato yakusanywe kupitia mfumo wa kisasa wa eleckroniki.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: