Kampuni ya simu inayoongoza nchini Vodacom Tanzania Plc, imepokea kwa furaha tangazo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (Tanzania Communications Regulatory Authority) ambapo Vodacom imepewa masafa ya kuongeza nafasi ya kuboresha na kuwafikia mamia ya wateja wake baada ya mnada uliofanyika tarehe 08 Juni 2018.

““Mgao wa eneo la mawasiliano ni hatua ya kimaendeleo kwa taifa na kwa uchumi. Ni jambo la kuleta mabadiliko makubwa kwa mtazamo wa upatikanaji wa mawasiliano na matumizi ya wigo wa mawasiliano uliopangwa utaiwezesha Vodacom kuchangia miundombinu ya mawasiliano ya simu ya mkononi ambayo ni kipengele muhimu cha maendeleo ya kiuchumi kama ilivyoelezwa katika Sera ya Taifa ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, 2016”, anasema Bw. Ali Mufuruki, Mwenyekiti wa Bodi ya Vodacom Tanzania PLC.

“Tunakaribisha taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na tumefurahia mafanikio yetu katika mnada huo na kuweza kupata wigo uliokuwa unahitajika kwa kiasi kikubwa katika mawasiliano. Hili linatuwezesha kuanza kutekeleza mipango yetu ya kuongeza kasi ya kupanua mtandao na utoaji wa mawasiliano ya kasi zaidi, tukitoa mawasiliano bora ya 4G nchi nzima,” amesema Bw. Diego Gutierrez, Afisa Mkuu wa Uendeshaji, Biashara ya Kimataifa wa
Vodacom.

Vodacom Tanzania PLC inaipongeza serikali kwa kusimamia mchakato na kuendesha mnada kwa mafanikio. “Ushiriki wetu kwenye mnada na mipango yetu ya kuwekeza kwenye mtandao wa 4G, vyote vinaonyesha dhamira tuliyonayo ya kutoa huduma bora nchini. Tunafurahi sana kutoa mchango wetu katika mipango ya maendeleo ya Tanzania,” alihitimisha Mufuruki.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: