Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori nchini (TAWA), Meja Jenerali mstaafu Hamisi Semfuko (wa pili kushoto mwenye miwani), akizungumza na walinzi wa wanyamapori katika maeneo yanayozunguka Pori ya Akiba la Maswa mkoani Simiyu alipokua akikagua shughuli za uhifadhi na ulinzi katika maeneo hayo juzi. WALINZI wa wanyamapori katika maeneo yanayozunguka Pori ya Akiba la Maswa yanayopakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wametakiwa kuwa makini na waadilifu kutokana na kuongezeka kwa wanyama adimu wanaofika maeneo yao.Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori nchini (TAWA) Meja Jenerali mstaafu Hamisi Semfuko alipokua akikagua shughuli za uhifadhi na ulinzi katika maeneo hayo.Meja Jenerali Semfuko, alisema kazi ya kupambana na ujangili inahitaji uvumilivu, uadilifu na ujasiri mkubwa kutokana na mazingira hatarishi yaliyopo."La muhimu kuna taatifa maeneo haya wameanza kuja wanyama adimu hivyo ningependa muongeze jitihada hizi mara dufu wanyama hao wasidhurike," alisema.Katika ziara hiyo wajumbe wa Bodi ya TAWA walipokea taarifa ya timu ya pamoja kati ya TAWA, Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), Frankfurt Zoological Society ( FZS), TAWIRI na Friedkin Conservation Fund (FCF) katika kuhifadhi na kulinda na kuhifadhi wanyama adimu.Taarifa hiyo iliyowasilishwa na wataalamu Philbert Ngoti wa TANAPA na Gerald Nyaffi wa FZS katika eneo la kitalu kilichopo Maswa Mbono kinachoendeshwa na kampuni ya Tanzania Game Tracker Safaris (TGTS).Wataalam hao walisema wamefanikiwa katika mradi huo kwa ufadhili wa familia ya Friedkin inayomiliki TGTS ililiyofadhili fedha, vifaa pamoja na helikopta, kazi ijayotarajiwa kuendelea katika maeneo mengine.Katika ziara hiyo TAWA  imeridhishwa na utendaji wa Makampuni ya uwindaji na upigaji picha za kitalii, yaliyopo katika maeneo yake kwa kusimamia uhifadhi na ulinzi pamoja na kuchangia miradi ya maendeleo ya wananchi yenye thamani zaidi ya sh 40 bilioni.Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori nchini (TAWA), Dk James Wakibara akizungumza na waandishi wa habari juu ya mchango kwa jamii, uhifadhi na kiuchumi wa  makampuni ya uwindaji wa kitalii zilizowekeza katika maeneo yao.Maeneo yaliyotembelewa na TAWA ni pamoja na Hifadhi ya Jamii ya Wanyamapori(WMA) ya Makao wilayani Meatu inayosimamiwa na kampuni ya Mwiba Holdings Limited.Dk Wakibara alisema, licha  mchango wa makampuni kwenye jamii, pia TAWA kupitia malipo ya kampuni hizo, imekuwa ikitoa takriban sh 6.5 bilioni kila mwaka kwa vijiji vyenye wawekezaji hao na halmashauri.Makampuni hayo yamewekeza katika baadhi ya maeneo ya vitalu 159 vilivyopo nchini na maeneo ya hifadhi za jamii za wanyamapori (WMA) 38 zilizopo nchini."Hizi kampuni za kitalii zina mchango mkubwa sana pia katika uhifadhi wa maeneo haya, hasa katika vita dhidi ya ujangili ikizingatiwa asilimia 95 ya maeneo yaliyohifadhiwa nchini yapo chini ya TAWA"alisema.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: