MAENDELEO BANK - PLC, inatarajia kufanya Mkutano mkuu wa 4 wa mwaka Mkutano huo utakaowakutanisha Wanahisa wote utafanyika Juni 23 mwaka huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.Hayo yametanabaishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank, Bwa. Ibrahim Mwangalaba alipokua akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Maendeleo Bank, uliopo makao makuu ya Banki, katika jengo la Luther House, siku ya jana jumatano .

Pamoja na taarifa hiyo Mwangalaba alifafanua dhamiria ya Banki katika kijitanua zaidi kwa kudumisha utendaji bora wa utoaji huduma hadi kufikia hadhi ya kitaifa jambo lililopelekea kutoa toleo jipya la hisa lililoanza tangu mwishoni mwa mwaka 2017.

Ifikapo tarehe 09 Septemba mwaka huu, Maendeleo Bank itakua inatimiza miaka 5 tangu kuanzishwa kwake.
Maendeleo Bank inaendelea Kutoka huduma kwenye matawi yake matatu ya yaliyopo Luther, Kariakoo na Mwenge. Pia inatoa huduma kupitia MB Mobile na zaidi ya ATM 270 za umoja nchi nzima.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: