Mkuu wa wilaya ya Misungwi, Juma Sweda (kushoto) akikagua shamba la pamba la Bw. Swalala Nteminyanda (kulia) katika kijiji cha Nyanh'onge wilayani  humo Juni 11, 2018. Ununuzi wa pamba kwa pesa taslimu wilayani  Misungwi unaendelea vizuri na kilo moja inanunuliwa kwa shillingi 1100/=. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Mkulima wa pamba katika kijiji cha Mondo wilayani Misungwi, Hoja Ngole akitumia mkokoteni wa kokotwa na ng’ombe kupeleka pamba yake kuuza kwenye Chama cha Ushirika wa Mwaniko katika kijiji cha Mondo Juni 11, 2018. Uuzaji wa pamba wilayani Misungwi unaendelea vizuri na kilo moja inauzwa kwa sh. 1100/=.
Katibu wa Chama cha Ushirika cha Msingi cha Mwanimo, Philip Makoye akionyesha pamba cha aliyoikataa na kuamuru ichambuliwe tena na mkulima aliyetaka kuiuza katika chama hecho wilayani Misungwi, Juni 11, 2018.
Wakulima wa zao la pamba Bibi Pendo Kitwala (katikati) na Sospeter Shija wakichambua pamba iliyokataliwa baada ya kugundulika kuwa ni chafu wakati walipotaka kuiuzwa katika Chama cha Ushirika cha Msingi cha Mwanimo wilayani Misungwi Juni 11, 2011. Ukaguzi wa hali ya juu unafanyika msimu huu wa uuzaji zao hilo ili kuwanasa wakulima wachache wanaojaribu kuuza pamba chafu. Lengo la hatua hiyo ni kurejesha heshima ya ubora na sifa nzuri ya pamba ya Tanzania katika soko la dunia. Kushoto ni Mussa Daudi akiwasaidia wazee hao.
Katibu wa Chama cha Ushirika cha Msingi cha Mwanimo, Phillip Makoye (kushoto) akipima katika mzani pamba ya Marco Masalamunda (watatu kulia) kwenye ghala la chama hicho cha msingi lililopo Katika jijini cha Mondo wilayani Misungwi Juni 11, 2018. Ununuzi wa zao la pamba kwa fedha taslimu unaendelea vizuri wilayani humo na kilo moja inanauliwa kwa shillingi 1100/=.

MKUU wa wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza, Bw. Juma Sweda amewataka wananchi wa wilaya hiyo kuhakikisha wanatumia vizuri fedha wanazozipata kutokana na mauzo ya zao la pamba.

Amesema ni vema wakatumia fedha hizo kwa ajili ya kujiletea maendeleo katika familia zao ikiwa ni pamoja na ujenzi wa nyumba bora na za kisasa na wawaendelea watoto kielimu.

Mkuu huyo wa wilaya ametoa agizo hilo leo (Jumatatu, Juni 11, 2018) wakati akiwa kwenye ziara ya kukagua shughuli za uvunaji na uuzaji wa zao la pamba. Ziara hiyo imefanyika kwenye vijiji vitatu vya kata ya Mondo wilayani hapa.

Bw. Sweda amesema wananchi wengi walihamasika kulima zao la pamba baada ya Serikali kuhamasisha walime na kuahidi kulifuatilia kuanzia hatua za utayarishaji wa mashamba hadi utafutaji wa masoko.

“Naishukuru Serikali kwani baada ya kuhamasisha ufufuaji wa kilimo cha zao la pamba nasi tuliungana na wananchi kuhakikisha maelekezo hayo tunayatekeleza kwa vitendo, lengo letu kubwa ni kuona zao hilo linarudi kama zamani,” amesema.

Amesema kwa sasa wapo katika hatua ya uvunaji na uuzaji, ambapo wamejipanga kukagua kikamilifu ili kuona zoezi hilo linaenda vizuri na pamba yote inayopokelewa na vyama vya Ushirika ni ile iliyo katika ubora unaohitajika

Amesema viongozi wa Vyama vya Msingi vya Ushirika (AMCOS) hukagua pamba kabla ya kuipokea na iwapo mkulima atabainika kupeleka pamba chafu hulazimika kuisafisha kwanza kwa kutenga safi na chafu ndipo hupima na kulipwa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: