Waziri wa Maji na Umwagiliaji Eng. Isack Kamwelwe akizungumza na waandishi wa jijini Dar es Salaam mapema leo kuelezea kutengua nafasi ya Kaimu Afisa mkuu wa DAWASA.

Na Cathbert Kajuna-Kajunason/MMG.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Eng. Isack Kamwelwe ametengua uteuzi wa aliyekuA kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Eng. Romanus Mwang'ingo na kuvunja bodi ya wakurugenzi wa DAWASA.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Eng. Kamwelwe amesema hatua hiyo imechukuliwa ili kupisha uchunguzi wa taarifa ya kuwepo kwa udanganyifu na ubadhirifu katika utekelezaji wa mradi wa kuchimba visima vya maji Kimbiji na Mpera huko Kigamboni jijini Dar es Salaam.

"Wakati jambo hilo linafanyiwa uchunguzi na TAKUKURU serikali imechukua hatua za kutengua uteuzi wa huyo Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu na Bodi yake kwa kushindwa kuchukua hatua stahiki ili kuunusuru mradi mapema," amesema Eng. Kamwelwe.

Taarifa hizi zinaonyesha pamoja na mambo mengine udanganyifu uliofanyika kuhusu idadi ya visima vilivyokamilika kama ambavyo zimewasilishwa wizarani na DAWASA na uhalisia katika eneo la utekelezaji wa mradi.

Aidha Waziri Eng. Kamwelwe amemteua Dkt. Sufian Masasi kukaimu nafasi hiyo mpaka utaratibu mwingine utakapokamilika.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: