Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI (NACP) kwa kushirikiana na TACAIDS na wadau wa USAID Tulonge Afya, inayofuraha kutangaza uzinduzi wa kampeni ya kitaifa inayoitwa Furaha Yangu. Kampeni hii inahamasisha mkakati mpya wa serikali wa Upimaji wa VVU na kuanza kutumia ARV mapema kwa wale watakao kutwa na VVU. Kupitia Furaha Yangu, ujumbe wa serikali ni kuwa kutambua hali yako ya VVU huleta amani, na kuanzishiwa ARV mapema kwa wale wenye VVU inawasaidia kuimarisha afya na kupunguza hatari ya kuambukiza VVU kwa wenza wao.

Katika dira ya kuwa na Taifa bila UKIMWI, Tanzania imeridhia malengo ya UNAIDS ya 90-90-90: ambapo 90% ya watu wote wanaoishi na VVU kutambua hali zao za VVU, 90% ya watu wote wenye VVU kuanza ARV, na asilimia 90 ya wote walionza ARV kupunguza kiwango cha VVU mwilini. Uzinduzi wa kampeni ya furaha Yangu – ambayo imekuwa ikiandaliwa kwa mienzi kadhaa na Wizara kupitia NACP kwa kushirikiana na TACAIDS, mradi wa USAID Tulonge Afya na wadau wengine ni mchango muhimu katika kutimiza malengo haya.

Kampeni ya furaha Yangu itazinduliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Mjaliwa Kassim Majaliwa (Mb), siku ya tarehe 19 Juni 2018, katika Jiji la Dodoma ambayo pia ni kutakuwa na siku tano za kutoa huduma za afya bila malipo ikiwemo huduma ya upimaji wa VVU kuanzia tarehe 19 June 2018. Wizara kupitia NACP pamoja na TACAIDS inatoa wito kwa wakazi wote wa Jiji la Dodoma na mikoa ya jirani kushiriki katika uzinduzi huu na kupima afya zao na kuonyesha dhamira yao ya kumaliza VVU na UKIMWI nchini.

Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Simu: +255 – 026 - 2323267,S.L.B 743, Dodoma
 
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: