Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isack Nchunda akiongea wakati wa kutangaza kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango kupitia kitengo chake cha (Government Electronic Payment Gateway) katika kutoa suluhisho la malipo rahisi ya papo kwa hapo kupitia huduma ya Airtel Money. Kushoto ni Ofisa mwakilishi wa GePG kutoka wizara ya Fedha na Mipango Basil Baligumya na Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando.
Ofisa mwakilishi wa GePG kutoka wizara ya Fedha na Mipango Basil Baligumya akiongea wakati wa kutangaza kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango kupitia kitengo chake cha (Government Electronic Payment Gateway) katika kutoa suluhisho la malipo rahisi ya papo kwa hapo kupitia huduma ya Airtel Money. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isack Nchunda na Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Jackson Mmbando.

Na Mwandishi Wetu.

Kampuni ya simu za mkononi Airtel Tanzania imezindua mfumo wa malipo wa kielekroniki kwa huduma za serikali utakaowezesha wateja wa mtandao huo zaidi ya milioni 10 kufanya malipo ya bili mbalimbali kupitia huduma ya Airtel Money.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Tanzania, Isack Nchunda amesema mfumo huo utatoa suluhisho la malipo rahisi ya papo kwa papo kupitia huduma ya Airtel Money.

“Idadi ya wateja wa Airtel Money inakua siku hadi siku na hivyo kufanikisha moja kati ya malengo ya serikali kuhakikisha kuwa inafanikisha upatikanaji wa huduma za kifedha kila mahali yaani mjini na vijijini. Nachukua fursa hii kuwaomba watanzania kutumia mfumo huu kwani ni salama,” amesema Nchunda.

Mfumo wa GePG ni kwa ajili ya kila mtanzania. “Nachukua fursa hii kuwaomba watanzania kutumia mfumo huu kwani ni salama, rahisi na nafuu”, alisema Nchunda huku akiongeza kuwa Airtel Tanzania imedhamiria kuendelea kuhudumia wateja kwa ubora wa hali ya juu kwa kuongeza idadi ya mawakala wa Airtel Money ambao kwa sasa wanafikia zaidi ya elfu 55.”Vile vile, tunaendelea kuongeza mawakala kupitia usambazaji wa vioski vya Airtel Money na kuongeza uekezaji katika maduka ya Airtel Money Branch ambayo sasa tayari yanatoa huduma kama wakala wa kawaida na pia kama wakala mkubwa ambapo hadi sasa hivi tumeshafungua matawi (Airtel Money Branch) zaidi ya 300 yanayotoa wigo mkubwa zaidi wa mawakala nchini.

Naye  Ofisa mwakilishi wa GePG kutoka wizara ya Fedha na Mipango Basil Baligumya amesema hadi sasa taasisi za serikali takribani  ya mashirika na taasisi 260 zimejisajili kwenye mfumo huo ikiwemo Halmashauri, Brela, Tanesco, Dawasco.

“Mfumo huo wa serikali kwa ajili ya kulipia huduma zote za serikali, kumrahisishia mwananchi kulipa kupitia mitandao ya simu, unatengeneza namna ambayo inafanana katika kulipia huduma zote za serikali kwa taasisi zilizounganishwa ikiwemo halmashauri, huduma za umeme, maji.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: