Watu watano wanadaiwa kufariki dunia usiku katika ajali iliyohusisha lori pamoja na gari dogo aina ya Noah eneo la mteremko wa mlima Igawilo nje kidogo ya jiji la Mbeya.

Mashuhuda wa tukio ambao walikuwepo wamesema kwamba huenda chanzo cha ajali hiyo ni lori ambalo liliferi breki na kuzigonga gari nyingine tatu zikiwemo za TANESCO na kampuni ya CocaCola pamoja na hiyo Noah ambayo ilikuwa na abiria watatu ambao wawili inahofiwa wamefariki papo hapo na mmoja amekimbizwa hospitali rufaa ya Mbeya kupatiwa matibabu.

Dereva wa lori na msaidizi wake wanahofiwa kwamba wamefariki dunia papo hapo na juhudi za kuondoa maiti zao zimekua zikiendelea wakati wa kutuma taarifa hii.

Ajali hii imekuja masaa machache tu baada ya waziri mpya wa Mambo ya Ndani Mhe. Kangi Lugola kumaliza ziara yake mkoani Mbeya ambapo pamoja na mambo mengine amevunja kamati na mabaraza ya usalama barabarani nchi nzima kwa nia ya kujipanga upya katika kupambana na jang hilo sugu la Taifa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: