Na Agnes Francis, globu ya jamii.

Ikiwa zimebaki dakika chache Azam FC kukutana na gormahia ya nchini Kenya kumenyana katika mchezo wa nusu fainali wa Kagame Cup (cecafa)

Mtanange huo utakoakuwa wa aina yake huku kila timu ikiitaji matokeo mazuri ya kushinda ili kusonga mbele zaidi,

Timu hizo zitaingia dimbani majira ya saa 8 mchana katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam

Wapinzani hao walishawahi kukutana katika fainali ya kuwania kombe hilo mwaka 2015 na azam kuibuka kidedea kutoka kifua mbele kwa kumcharaza gor mahia mabao 2-0.

Mabingwa watetezi hao Azam FC wajinadi kujipanga vema kuhakikisha wanatetea taji lao kwa maandalizi zaidi ya wachezaji chini ya kocha wao mpya kutokea singida united ambaye awali alikuwa akikinoa kikosi cha yanga sc, van pul jin raia wa uholanzi.

Akizungumza afisa habari wa Azam FC,  Jaffary Maganga  (pichani) amesema kuwa gemu hiyo itakuwa ni ya ushindani zaidi kwa pande zote mbili kutafuta nafasi nzuri zaidi.

"Kikosi kimejipanga vizuri kupambana dhidi ya wapinzani wetu gor mahia ukizingatia pia wenzetu pia wako vizuri na wanawacheza wazuri,ila tutahakikisha tunapata matokeo mazuri" amesema Jaffary.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: