Msajili wa Chuo cha ustawi wa jamii Nuru kalufya akizungumza na blogu ya jamii juu ya mkakati walioweka katika kudahili wanafunzi wapya 2018/2019.

Na Leandra Gabriel, Blogu jamii

CHUO cha ustawi wa jamii kilichopo Kijitonyama jijini Dar es salaam kimeanza kudahili wanafunzi kwa mwaka 2018/2019 katika maonesho al maarufu kama maonesho ya TCU yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi mmoja.

Akizungumza na Michuzi blog Msajili wa Chuo hicho bi. Nuru Kalufya ameeleza kuwa wamejipanga katika kupokea wanafunzi katika msimu huu na wanasajili kupitia mtandao (online) bure kabisa kinachohitajika ni wanafunzi kuwa na vyeti vyao na namba zao za usajili (index number) na watapata huduma hiyo ya udahili na ushauri wa kitaaluma bure kabisa.

Kuhusiana na kozi zinazotolewa na Chuo hicho bi. Nuru ameeleza kuwa wanatoa kozi tano kwa gharama nafuu kabisa na hii ni kuanzia ngazi ya cheti, stashahada, shahada, uzamili na post graduate ya kozi ya Health System Management ambayo ni mpya kabisa chuoni hapo.

Kuhusiana na usajili wa Chuo bi. Nuru ameeleza kuwa wamesajili na wanatambulika na Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) pamoja na NACTE na Serikali kwa ujumla hivyo wazazi na wadahiliwa wasiwe na hofu.

Aidha ameeleza kuwa watatoa huduma katika maonesho hayo hadi kesho majira na saa kumi na moja jioni na baadaye wataendelea kutoa huduma hizo katika chuo chao kinachopatika Kijitonyama hivyo wanafunzi waendelee kujitokeza kwa wingi zaidi.

Naye mshauri wa wanafunzi bi. Silvia Ngiga amewahakikishia wanafunzi usalama pindi wawapo shuleni na wanafunzi watokao mikoani watapata huduma za malazi na huduma nyingine za kijamii ni za kuaminika katika chuo hicho.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: