Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akikabidhiwa vikombe na Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Elimu Mhandisi Joyce Baravuga waliyoshinda vijana wa shule za msingi na sekondari Mkoa wa Morogoro katika mashindano ya UMISETA na UMITASHUMITA yaliyofanyika jijini Mwanza Juni Mwaka huu. Kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw. Clifford Tandari
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akikabidhiwa na Katibu Tawala Msaidizi - Elimu Mhandisi Joyce Baravuga kikombe kati ya vikombe nane walivyoshinda kwenye mashindano mablimbali ya michezo ya UMISETA NA UMITASHUMTA yaliyofanyika Mkoani Mwanza. Kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw. Clifford Tandari.
Katibu Tawala wa Mkoa Morogoro Bw. Clifford Tandari akizungumza jambo kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Kebwe Stephen Kebwe ili kukabidhiwa vikombe hivyo.
Katibu Tawala wa Mkoa Morogoro Bw. Clifford Tandari akizungumza jambo kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Kebwe Stephen Kebwe ili kukabidhiwa vikombe hivyo.

Na Andrew Chimesela – Morogoro.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe amewapongeza vijana wa shule za Msingi na Sekondari Mkoani humo walioshiriki mashindano ya michezo kwa shule za msingi na Sekondari (UMITASHUMTA na UMISETA) na kuuletea heshimu Mkoa wa Morogoro kwa kurudi na vikombe kutokamna na kushinda michezo mbalimbali.

Dkt. Kebwe ametoa pongezi hizo Julai 6 mwaka huu wakati akikabidhiwa vikombe zaidi ya nane vya ushindi wa michezo mbalimbali ya UMITASHUMTA na UMISETA iliyofanyika Mwezi Juni mwaka huu katika viwanja vya Chuo cha Ualimu cha Butimba Jiji la Mwanza.

Dkt. Kebwe amesema Mkoa unatakiwa kujipanga na kuweka utaratibu wa kuendeleza vipaji vya vijana wanaoleta heshima ya Mkoa ili waweze kufanya vizuri zaidi. “kwa hiyo hawa vijana tuwalee vizuri na tuwatunze vizuri wakiwemo vijana hawa ambao wako Kizuka Ngerengere wanafanya vizuri sana, heshima hii ambayo wanatuletea tuone namna ya kuendeleza” alisema Dkt. Kebwe.

Hata hivyo Mkuu huyo wa Mkoa alimuagiza Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw. Clifford Tandari pamoja na Halmashauri zote za Mkoa huo kwa jumla kuanza kujipanga upya kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya michezo hiyo ili mwakani Mkoa uingie kwenye tatu bora au zaidi kwa mashindano yote ya Shule za Msingi na Sekondari.

Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Elimu Mhandisi Joyce Baravuga aliwashukuru wajumbe wa Sekretarieti ya Mkoa wa Morogoro, viongozi wa ngazi ya Wilaya, vijana walioshiriki mashindano hayo pamoja na walimu na wadau wote wa michezo Mkoa wa Morogoro kwa ushirikiano mkubwa waliouonesha hadi kufanikisha Mkoa kupata mafanikio hayo.

Naye Afisa michezo Mkoa wa Morogoro Grace ….amesifu utaratibu wa mashindano ya mwaka huu ya kuwa na kambi mbili za wanamichezo tofauti na mwaka jana, amesema kuwepo na kambi mbili ya Chuo cha Butimba na ile iliyowekwa katika shule ya sekondari ya Nsumba, imeondoa changamoto nyingi zilizokuwa zinajitokeza ingawa amesema suala la bajeti kwa mashindano hayo bado ni changamoto.

Mkoa wa Morogoro katika mashindano hayo kitaifa umeshika nafasi ya tisa kwa shule za sekondari kati ya mikoa 28 ya Tanzania bara na Visiwani ukilinganisha na mwaka jana ambapo ilishika nafasi ya 15. Kwa upande wa shule za msingi Mkoa umeshika nafasi ya 5 kati ya mikoa 26 ya Tanzania bara ambapo mwaka jana pia ilishika nafasi hiyo kitaifa.

Kwa Mujibu wa Mhandisi Joyce, mashindano hayo yaliyofanyika kuanzia Juni 3 hadi Juni 29 mwaka huu Mkoani Mwanza, Mkoa umeshinda mshindi wa kwanza kitaifa Mpira wa kengele, mshindi wa pili wasichana mpira wa kengele, mshindi wa tatu kitaifa wavulana mpira wa mikono, na mshindi wa tatu kitaifa kwa upande wa ngonjera.

Kwa upande wa Riadha, Mkoa umeshinda mshindi wa kwanza mita 200 wavulana, mshind wa pili mita 200 wasichana, mshindi wa tatu mita 100 wasichana na mshindi wa pili kitaifa kurusha mkuki wavulana. Wakati huo mwalimu wa mpira wa kengele amekuwa kocha bora kitaifa na alipewa zawadi ya simu ya mkononi kutoka kampuni ya i – tel.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: