Waumini na Viongozi wa Kanisa la The Pool of Siloam la Jijini Mbeya wakifanya maombezi maalumu katika eneo ambalo ajali ilitokea na kusababisha vifo vya watu 20 na wengine 45 kujeruhiwa katika Mteremko wa Mlima Iwambia - Mbeya.
Waumini wa Kanisa la The Pool of Siloam la Jijini Mbeya, leo wamekusanyika na kufanya maombi maalumu katika eneo la Mlima Mbalizi, ambalo hivi karibuni ilitokea ajali naada ya magari manne kugongana na kusababisha vifo vya watu 20 na majeruhi 45.

Waumini hao wakiwa wameongoza na kiongozi wao, Kuhani Wisdom Shangwe, wamesema lengo la maombi hayo ni kuzuia jinamizi la ajali lililoukumba Mkoa wa Mbeya.

Akizungumza baada ya maombi hayo, Kuhani Shangwe, amesema licha ya serikali kuweka mikakati ya kuhakikisha ajali zinatokomea kuna nguvu ya ziada inahitajika ya kukemea mapepo.

“Mkoa wa Mbeya kwa sasa umekumbwa na mfululizo wa matukio ya ajali na kumwaga damu za watu wasio na hatia hivyo makanisa yana wajibu wa kutetea roho hizo pamoja na kuzuia mapepo ambayo yanatumiwa na baadhi ya watu kwa maslahi yao binafsi.

“Kanisa lina jukumu la kuombea viongozi wa nchi akiwamo rais na wasaidizi wake ambao ni mawaziro, wakuu wa mikoa, wilaya na wengine,” amesema.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: