Mahakama Kuu ya Kenya imemhukumu KUNYONGWA HADI KUFA Bi Ruth Wanjiru Kamande mwenye miaka 24 baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake Bw Farid Mohammed kwa kumdunga kisu mara 22 mwaka 2015.

Ruth ambaye ameshinda taji la Miss Lang'ata Prison alipokuwa mahabusu, ameiomba radhi familia ya Mohammed kwa kitendo hicho cha kushindwa kuzuia hasira zake zilizopelekea kumdunga kisu mpenzi wake. Amewasihi wamsamehe kabla ya hukumu yake ya kunyongwa kutekelezwa kwani anajutia makosa yake.

Ruth alikiri mbele ya mahakama kutekeleza shambulio hilo baada ya kukuta ujumbe wa mapenzi kwenye simu ya mpenzi wake kutoka kwa mwanamke mwingine.

Tangu Kenya kuandika katiba mpya, Magereza nchini humo yameimarishiwa miundo mbinu muhimu sambamba na kuhakikisha kuwa wafungwa wawapo gerezani wanapata haki zao za binadamu. Haki hizi ni pamoja na chakula bora, maji safi, malazi mazuri, mahusiano mema kati ya mfungwa na askari jela, habari na kuendeleza vipaji mbali mbali vya wafungwa miongoni mwa haki zingine za binadamu.
Mrembo Ruth Wanjiru Kamande akipanda juu ya jukwaa katika gereza la Lang'ata kuwania taji la Miss Lang'ata Prison mwaka 2016.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: