Mwanamke kwanza unatakiwa uwe na akili nzuri.
Akili nzuri huanza ktk kumjua Mungu.

Unaposoma neno la Mungu na kutafakari lazma uwe na akili nzuri.

Ili uwe na akili njema lazma uzishike na kukubali sheria za Mungu.

Mwanamke aliyeolewa lazma azishike na kukubali sheria za Mume,

Lazma matendo yenu na mienendo yaendane,lazma mufanane ili mutembee pamoja,hamwezi kaa pamoja kama hamfanani.

Mwanamke aliyeolewa amefungwa na sheria ya mumewe pindi mumewe akiwa hai.

Wanawake wengi hubomoa nyumba zao kwa mikono yao wenyewe,nasema wanawake wengi na sii wanaume ieleweke ivyo.

Mwanamke unaishi na mume kweli waweza mwandalia mmeo maji bafuni bila sabuni?ni akili ya wapi hiyo?
Kushindwa kutambua majukumu yako kama mama?

Mwanamke umeolewa wataka kumzimisha mmeo sauti hapo ndani yani utaki mumeo haoji anapo ona hapako sawa,je kichwa cha familia ni mke au mume?

Mwanamke uliye olewa ujui nyumba za kuabudu wewe kutwa vibarazani ,umefundishwa wapi tamaduni mbovu na za ovyo ivyo?

Mwanamke amchaye Mungu ndiye atakayesifiwa,

Sasa wewe endelea kurukaruka kama kunguru anayetafuta nyama ziko wapi katika machinjio.

Mwanamke uliyeolewa unatakiwa uwe kama tai na si kunguru.

Mwanamke umeolewa unakua na mdomo mchafu katika nyumba yako,unashindwa kuwakirimia wageni,alafu unajiita mama Wa familia?
Woooooi mwanamke anapaswa awe na maneno matamu kama asali,na mazuri kama dhaabu,na si mabaya kama shubiri.

Mwanamke umeolewa unakuwa na roho mbaya, umbeya, majungu, visirani.

Alafu leo na kesho mumeo amechoka kero zako kwa nini asichepuke?

Aliyempa nafasi ni nani kama si wewe mwanamke? Anayevunja nyumba yake ni nani kama si wewe mwanamke?

Unashindwa mwandalia mmeo maji na sabuni aoge ? Akiona Barbara kubwa ina jamu akaamua achepuke utamlaumu nani?

Mwanaume akiona mwanamke una hila una visasi una chuki una umimi?
Nani anavunja nyumba kama si wewe mwanamke uliyekosa akili?

Mwanamke unashindwa kumwomba Mungu akuongoze unaomba marafiki na ndugu wakuongozee familia?

Mtumaini bwana kwa moyo wako wala usizitegemee akili zako mwenyewe,
Sasa uko kukopa akili za watu mnatoa wapi?

Ukitegemea akili yako mwenyewe au ya rafiki kutakupeleka kubaya,
Na akili yako ikiwa imara uwezi kuwa nguzo ya chumvi.

Ni vyema ukachanganya akili yako na ya Mungu ili uwe na kibali cha kuongoza familia,kuishi na watu,cha kuwajali Wa kwenu,cha kupambana na changamoto,cha kuvuka majaribu salama,cha kuwa mama bora,cha kupata hekima,akili,na maarifa.

MWANAMKE AMCHAYE BWANA NDIYE ATAKAYESIFIWA. ANZA NA MUNGU KILA JAMBO.

Utakua mlinzi bora ktk familia,
Utakuwa mjeshi haswa,
Utaweza kumtunza na kumlinda mumeo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: