Ukiona watu wanafanya vizuri katika mitihani yao tambua kuwa walifanya maandalizi au walijiandaa vizuri. Ukiona ndege inaruka na kutua salama basi tambua kuwa maandalizi ya kuruka yalikuwa mazuri hata maandalizi ya kutua yalikuwa mazuri.

Haya ni baadhi mambo ninayo weza kuyatolea mfano lakini kikubwa ninataka kukumbusha umuhimu wa maandalizi.

Najua una mipango mingi itokanayo na ndoto kubwa uliyonayo lakini mipango pekee bila maandalizi haiwezi kukuletea matokeo mazuri usiwe na haraka kwa kuona kuwa unapoteza muda kufanya maandalizi hapana, maandalizi ni muhimu sana na hayapelekei upotevu wa muda.

Ndugu Less Brown aliwahi kusema, “ukinipa kazi ya kukata mti nitatumia muda mwingi kunoa shoka kwanza” hii ni dhahili kuwa kunoa shoka ni maandalizi mazuri ya kukata mti hii inaonyesha kuwa maandalizi ni muhimu na hupunguza tabu zisizo za lazima lakini pia yatakusaidia kuokoa muda pia.

Ukiona watu wanaenda shule kwanza kabla ya kazi tambua huko ni kujiandaa. Yamkini wangeweza kwenda kazini moja kwa moja lakini ingewachukua mud asana. Kuwa na ufanisi mzuri. Maandalizi shuleni humsaidia mwanafunzi kupata uzoefu au ujuzi uliofanyiwa tafiti nyingi na kwa muda mrefu lakini yeye huupata ndani ya muda mfupi hii ni dhahili kuwa maandalizi yatakusaidia kutembea umbali mrefu ambao ungetembea kama ungeanza moja kwa moja maandalizi yatakusaidia kuvunja vunja changamoto ambazo yamkini zingekusumbua na kukukatisha tamaa.

Nikweli mipango yako ni mizuri , ndoto yako ni kubwa na yenye tija si kwako tu na hata kwa watu wengine lakini zingatia hatua ya maandalizi ili ufanye vizuri Zaidi.

Usilie usinung’unike wala kukata tamaa yamkini mambo yako yote yamekaa sawa lakini fanya jambo moja tu sasa ili uingize kwenye ahadi yako na kuitawala vizuri,

JIANDAE USHIND NI LAZIMA!!!
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: