Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Senyamule akiwa katika picha ya pamoja na vijana waliojitokeza katika ufunguzi wa mazoezi yatakayokuwa yanafanyika kwa wiki mara moja.
 Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Senyamule akiongea machache wakati wa ufunguzi wa mazoezi yatakayokuwa yanafanyika kila wiki mjini Same, Kilimanjaro.
Hiari yashinda utumwa, ni maneno yaliyoonekana kusemwa na wanasame baada ya kupokea taarifa inayoonyesha athari za magonjwa yasiyoambukiza ambayo mengi yanatokana na kutofanya mazoezi na Kutokula vyakula sahihi.

Mratibu wa michezo aagizwa kupanga ratiba ya kufanya mazoezi kila wiki wakati wananchi waagizwa kufanya mazoezi nusu saa kila siku.

Vijana waonyesha mwamko kuliko watu wazima. Mkuu wa Wilaya ya SAME, Rosemary Senyamule amewataka wahusika wanaosimamia mazoezi hayo kutoa elimu kwa muda wa nusu saa kila baada ya kuanza mazoezi ili kuongeza mvuto wa watu kuja kwenye mazoezi.

Mada zenye nguvu kujadiliwa ikiwa ni pamoja na kusikilza kero.
" Same is not same"
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: