Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Amina Masenza (wa kwanza kulia) ramani ya maeneo yanayopata mawasiliano mkoani humo wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Miundombinu ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano kwenye mkoa huo. Anayeshuhudia katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Hawa Mchafu.
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kushoto) akiteremka kwenye kilima kilichojengwa mnara wa mawasiliano wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Miundombinu ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano kwenye kijiji cha Mkulula kilichopo Kata ya Malenga Makali mkoani Iringa. Wa pili kulia ni mjumbe wa Kamati hiyo Mhe. Bhagwanji Meisuria
 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Hawa Mchafu akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati hiyo na watendaji (hawapo pichani) kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Amina Masenza (wa kwanza kushoto) wakati wa ziara ya Kamati hiyo ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano kwenye mkoa huo. Wa kwanza kulia ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akisaini kitabu cha wageni
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akifafanua jambo kwa wananchi wa kijiji cha Mkulula kilichopo Kata ya Malenga Makali mkoani Iringa wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Miundombinu ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano kwenye mkoa huo. Wa pili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Hawa Mchafu na wa kwanza kulia ni mjumbe wa Kamati hiyo Mhandisi Ramo Makani
 Mwenyekiti wa kijiji cha Mkulula kilichopo Kata ya Malenga Makali mkoani Iringa Bwana Samwel Mbande akiishukuru Kamati ya Bunge ya Miundombinu kwa kufika kijijini hapo wakati wa ziara yao ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano kwenye mkoa huo. Wa kwanza kulia ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye na wa tatu kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Hawa Mchafu
Wanakiji wa kijiji cha Mkulula kilichopo Kata ya Malenga Makali mkoani Iringa wakimsikiliza Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (hayupo pichani) kuhusu jitihada za Serikali za kuwapatia wananchi mawasiliano wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Miundombinu kwenye kijiji hicho ya ukagua upatikanaji wa mawasiliano.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeyataka makampuni ya simu nchini kutoa huduma za data kwa wananchi waishio vijijini na maeneo yasiyo na mvuto wa kibiashara ambapo makampuni hayo yamejenga minara kwa ajlii ya kuwapatia wananchi mawasiliano

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Ndiye wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Miundombinu ya kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano kwa wananchi waishio viijijini na maeneo yasiyo na mvuto wa kibiashara wakati akizungumza na wanakijiji wa kijiji cha Mkulula kilichopo Kata ya Malenga Makali mkoani Iringa

Nditiye amefafanua kuwa kampuni za simu zinatoa huduma ya sauti tu yaani 2G kwenye minara ya mawasiliano waliyojenga badala ya kutoa huduma ya data kwenye maeneo hayo ili wananchi wapate huduma ya intaneti. Amesema kuwa Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) inatoa ruzuku kwa makampuni hizo ili wajenge minara. “Tunataka wananchi wapate mawasiliano kwa kuwa wanalipia na ni haki yao ya msingi kuwasiliana na hii ndio Serikali ya Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuhudumia wananchi wa hali zote,” amesema Nditiye. 

Ameongeza kuwa hadi sasa UCSAF imetoa ruzuku kwa makampuni ya simu ambapo jumla ya kata 530 zimepatiwa huduma ya mawasiliano kwenye maeneo mbali mbali nchini na ujenzi wa mnara mmoja una gharimu kati ya kiasi cha shilingi milioni mia mbili hadi milioni mia tatu.

Akiwa katika ziara hiyo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Hawa Mchafu amesema kuwa makampuni ya simu yanapowekeza yasiwekeze kwa mahitaji ya kipindi kifupi bali miundombinu ya mawasiliano wanayojenga izingatie mahitaji ya muda mrefu kwa kuwa wananchi wanaongezeka kwenye maeneo hayo na wanakuwa wengi mathalani kwenye eneo la kata hiyo wananchi wananchi wanafanya shughuli za uchimbaji wa madini, kilimo na ufugaji wa samaki. 

Ameongeza kuwa watoa huduma waweke mawasiliano ya data yaani 4G ili wananchi wapate huduma. “Haiwezekani fedha imetolewa na Serikali ya kujenga mnara kiasi cha shilingi milioni 260 halafu wananchi hawawasiliani,” Mhe. Mchafu amesema. Amefafanua kwa wanakijiji hao kwa kusema kuwa, “mnara mnauona umejengwa na TIGO kwa kupatiwa ruzuku na Serikali kupitia UCSAF kiasi cha shilingi milioni 260, nawaomba muiamini Serikali kuwa itatua kero zenu” Mhe. Mchafu amesema. 
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: