Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel akieleza jambo mara baada ya kupokea maelezo juu ya mradi wa umwagiliaji maji shambani kwa kutumia TEHAMA.
Mmoja wa wafanyakazi wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere akitoa maelezo kuhusiana na programu za chuo kwa Wananchi waliotembelea banda hilo.
Mhadhiri wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere , Samwel Lunyelele akitoa maelezo kwa wakazi wa Jijini Dar es Salaam waliotmebela banda la chuo hicho katika Maonesho ya 42 ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waliotembelea Banda la Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere wakiangalia historia ya chuo.

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Gabriel amewataka Vijana kuendelea kuwa wabunifu kwa kutumia teknolojia ya Ict ili waweze kuleta tija katika mapinduzi ya uchumi wa Viwanda.

RC Gabriel amesema hayo mapema leo jijini Dar es Salaam alipotembelea banda la Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere lililopo katika Maonesho ya 42 ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam na kujionea ubunifu wa umwagiliaji maji shambani kwa kutumia teknolojia ya mfumo wa TEHAMA uliofanywa na Wanafunzi wa Chuo hicho.

“Nahitaji kuona project hii ikihamishiwa katika shamba kubwa la ekari tano, na mimi niko tayari kutumia teknolojia hii katika mkoa wangu wa Geita ili kusaidia Kilimo cha umwagiliaji” amesema Rc Gabriel.

Rc Gabriel aliendelea kwa kukipongeza Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwa kuendelea kuwa wabunifu na kusimamia fikra za Mwasisi wan chi hii Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: