Rais wa Umoja wa Wanamuzi Tanzania (TAMUFO), Dk.Donald Kisanga akiwa na mmoja wa maofisa waandamizi wa DiGiSPICE Company East Africa Nairobi baada ya kukutana Parlands Nairobi kwa ajili ya kujadili changamoto za wanamuziki wa Tanzania katika soko la Afrika Mashariki na Dunia kwa ujumla.
Rais wa Umoja wa Wanamuzi Tanzania (TAMUFO), Dk.Donald Kisanga na Katibu wake, Stella Joel (kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na maofisa waandamizi wa kampuni hiyo baada ya kuwatembelea ofisini kwao wiki iliyopita.

Na Dotto Mwaibale.

RAIS wa Umoja wa Wanamuzi Tanzania (TAMUFO), Dk.Donald Kisanga na Mkurugenzi wa DiGiSPICE Company East Africa Nairobi wamekutana Parlands Nairobi kwa ajili ya kujadili changamoto za wanamuziki wa Tanzania katika soko la Afrika Mashariki na Dunia kwa ujumla.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam, Dk.Kisanga alisema katika mkutano huo uliowakutanisha viongozi kutoka nchi 12 za Afrika wamepata fursa nyingi na mbinu za kuwasaidia wanamuziki kupata faida kutokana na kazi zao.

"Tumezungumza mambo mengi na uongozi wa kampuni hiyo inayojishughulisha na kuuza nyimbo za wanamuziki kwa njia ya mitandao kama You Tube, Amazon's, Itunes na Spotify ambayo inauzoefu mkubwa wa kazi hiyo" alisema Kisanga.

Kisanga alisema matunda ya kuhudhuria mkutano huo mkubwa wa kimataifa yametokana na mkutano mkubwa walioufanya mapema mwaka huu na Digispice Tanzania uliofanyikia jijini Dar es Salaam na kuwashirikisha wanamuziki wa Dansi, Bongoflava, Taarabu, Gospel, muziki wa Asili na Kaswida.

Alisema mkutano huo ulihudhuriwa na mgeni rasmi Mbunge Martha Mlata ambaye aliongozana na Inspekta wa Polisi Dk. Ezekiel Kyogo anayeshughulikia masuala ya sheria TAMUFO.

"Napenda kuwaambia wanamuziki wakae mkao wa kula kwani ni hakika kwamba TAMUFO kipo kwa ajili ya kuwakomboa wasanii wa Tanzania
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: