Washindi 10 wa kupitia bia rasmi ya Tanzania katika mashindano ya soka ya kombe la Dunia yanayoendelea, wamereja nchini jana na wameielezea safari hiyo kuwa mbali na kuwawezesha kupata burudani ya soka mubashara pia wameweza kufanya utalii yenye vivutio nchini humo.

Mmoja wa washindi hao, Leodgard Isaac kutoka Dar es Salaam, akiongea kwa niaba ya wenzake alisema kuwa safari hiyo imewawezesha kutimiza ndoto yao ya kuona mashindano hayo makubwa ya soka moja kwa moja kutoka viwanjani na kuwaona wachezaji na makocha wengi maarufu duniani sambamba na kuungana na mashabiki wa soka kutoka nchi mbalimbali duniani na kuitangaza Tanzania kupitia bia ya Kilimanjaro
“Safari hii imetuwezesha kuona mambo mengi ambayo hatukutegemea kuyaona maishani ,tunashukuru bia ya safari kwa kubuni promosheni hii ambayo mbali na kutuwezesha kupata burudani ya michezo tumeweza kutembelea sehemu mbalimbali za utalii nchini Urusi na imetukutanisha na watu wengi na kupata marafiki wengi wapya pia tumeweza kutembelea ofisi za ubalozi wa nchi yetu nchini humo”alisema.

Kwa upande wake, Meneja Masoko na Udhamini wa TBL Group ambaye aliongozana na washindi hao, George Kavishe, alisema kuwa safari hiyo imeenda vizuri na washindi wameifurahia “Tunafurahi dhamira yetu ya kuwapatia burudani wateja wetu katika msimu huu wa kombe la dunia 2018 imefanikiwa na tutaendelea kubuni promosheni mbalimbali zenye mwelekeo wa kunufaisha wateja wetu”,alisema.
Kavishe, alisema promosheni inaendelea kwa wateja kujishindia fedha taslimu shilingi milioni moja kwa wiki kwa wiki kumi,na muda wa maongezi wa simu wa shilingi 2,500/- ,kila wanaponunua bia ya Kilimanjaro na kushiriki mara (sita) 6 kutuma namba iliyopo chini ya kizibo kwenda 15451 fedha taslimu kiasi cha shilingi 1,000,000/- Kila wiki kwa wiki Kumi na tayari washindi 6 wamejishindia fedha taslimu na kuwataka wateja kuendelea kuichangamkia waweze kujishindia.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: