Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda amelishauri Shirika la ndege la Tanzania ( ATCL) kufanya kazi kwa pamoja na Bodi ya Taifa ya Utalii (TTB) kwa lengo la kuongeza idadi ya watalii wanaokuja nchini kwa shughuli za utalii.

Amesema TTB na ATCL wanategemeana sana katika utendaji wa kazi zao hivyo lazima wafanye kazi kama timu.

Amesema Taasisi hizo zikishirikiana kikamilifu zitachochea ukuaji wa uchumi kwa kuongeza idadi ya watalii wanaokuja nchini kwa kutumia ndege zetu.

"Kwa sasa tuna usafiri wa uhakika tofauti na mwanzo hivyo ni lazima tuone mabadiliko kwenye sekta ya utalii" alisema Mhe. Pinda.
Amewakikishia kuwa endapo watafanya kazi kwa umoja wataweza kufikia malengo makubwa na kupelekea nchi kuwa na uchumi wa kati.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, Ladsilaus Matindi amesema hadi hivi sasa wamekuwa na utaratibu wa kukutana na TTB mara mbili kwa wiki kwa lengo la kujadiliana na kupanga mikakati ya maendeleo baina yao.

Ameongeza kuwa hadi hivi sasa wameshapiga hatua kubwa kutokana na vikao ambavyo wamekuwa wakikutana.

Mkurugenzi Mkuu, Matindi amemhakikishia Mhe.Pinda kuwa ujio wa ndege mpya waliyoipokea hivi karibuni aina Boing 787-7 Dreamliner itachangia sana kuifungua Tanzania katika nyanja za kiuchumi kwa kuleta watalii wengi zaidi nchini.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: