Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Bwana Laurean Bwanakunu Rugambwa (kulia), akiwa na viongozi wenzake kutoka Wizara ya ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji na Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dar es Salaam leo wakati wakiupokea ujumbe wa wawekezaji wa sekta ya Afya kutoka kampuni ya Kimataifa ya Fosun kutoka China, ambao wamekuja kuwekeza kwenye viwanda vya uzalishaji dawa na vifaa tiba.
Mkutano na wawekezaji hao ukiendelea.
Mkutano ukiendelea. Katikati kulia ni Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu na Waziri wa Viwanda, Charles Mwijage.
Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage (wa nne kutoka kushoto) na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (wa pili kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe huo kutoka China. Wa tatu kutoka kushoto ni Rais wa Fosun Pharma,Willium Yifang WU.

Na Dotto Mwaibale.

WIZARA ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji kwa kushirikiana na Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto wamepokea ujumbe wa wawekezaji wa sekta ya Afya kutoka kampuni ya Kimataifa ya Fosun kutoka China, ambao wamekuja kuwekeza kwenye viwanda vya uzalishaji dawa na vifaa tiba.


Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage (Mb.) ameeleza kuwa msimamo wa serikali ni kuhakikisha viwanda vinajengwa nchini ili kupunguza mzigo wa kununua dawa nje ya nchi kwa gharama kubwa,kupoteza ajira na pato la serikali.

Kwa upande wake,Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu amesema asilimia 94 ya fedha za bajeti zinazotengwa kwa ajili ya kununua dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara hupelekwa nje ya nchi,na asilimia 6 tu ndio hununua kutoka viwanda vya ndani. Hii ni kwa sababu hakuna viwanda vinavyoweza kuzalisha dawa tunazozihitaji.

Wataalamu walioshiriki majadiliano na wawekezaji hao ni pamoja na Bohari ya Dawa(MSD),Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA),Kituo cha Uwekezaji nchini(TIC), Mamlaka ya Uwekezaji (EPZ) na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC).

Rais wa Fosun Pharma, Willium Yifang WU amesema ili wawekeze wanahitaji ardhi ekari 10 kwa ajili ya kuanzisha kiwanda.

Kwa mujibu wa Waziri Mwijage wawekezaji hao wakiwa tayari serikali itawapatia eneo kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda hicho cha dawa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: