Na Agness Francis, Globu ya Jamii.

Msemaji wa Klabu ya Yanga Dismas Ten ametoa wito kwa mashabiki na wanachama wa Yanga kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Taifa katika mchezo wa marudiano dhidi ya Gor Mahia ya nchini Kenya.

Msemaji huyo amezungunza leo Jijini Dar es Salaam amesema kuwa Mchezo utakapigwa siku ya Jumapili katika Dimba la Uwanja wa Taifa ambapo utaanza majira ya saa moja usiku.

Katika muendelezo wa Michuano ya Shirikisho barani Afrika mpaka sasa Yanga haijafanikiwa kupata ushindi hata mmoja katika Kundi D lenye timu za USMA Alger, Gor Mahia, Rayon Sports.

Mchezo uliopita julai 18 nchini kenya mwaka huu, yanga haikuweza kufurukuta dhidi ya Gor mahia ambapo ilikubali kichapo cha mabao 4-0

Rekodi hiyo mbaya kwa Yanga imewafanya ibiruze mkia katika kundi lao kwa alama 1, vinara wao wakia ni Gormahia 5, wakifatiwa na Rayon sport ya nchini Rwanda 5, huku nafasi ya tatu ni USMA Alger akiwa na alama 4.

"Kikosi kimekita kambi yake mkoni Morogoro na leo walikuwa mazoezini katika uwanja polisi katika mandalizi ya mechi hiyo,wachezaji wameaahidi kushinda kuondoka na alama nyumbani 3 ili kufika pazuri zaidi "amesema Ten

Mchezo huo utakaokuwa wa aina yake na wenye mvuto ni kwa kiingilio cha shilingi 7000 kwa VIP na 5,000 kwa viti vya kawaida.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: