Na Mwandishi Wetu.

Kikosi cha Yanga kinatarajia kuondoka leo jijini Dar es Salaam kuelekea mkoani Morogoro kuweka kambi maalum dhidi ya Gor Mahia.

Yanga itakutana na Gor Mahia katika mchezo wa mkondo wa pili wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa Julai 29 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Yanga wamemua kuelekea Morogoro kwa ajili ya kupata utulivu kutokana na mazingira ya mkoa huo kuwa na utulivu wa aina yake pamoja na hali ya hewa tofauti na Dar es Salaam.

Safari hiyo imekuja mara baada ya viongozi wa juu kukutana na wachezaji wao jana katika makao makuu ya klabu hiyo ili kutatua masuala mbalimbali ikiwemo madai ya mgomo na hatimaye kufikia mwafaka wa kukubali kuendelea na mazoezi.

Katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Moi International Sports Center Stadium huko Nairobi Kenya, Yanga ilipoteza kwa idadi ya mabao manne kwa sifuri.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: