Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohamed Khamis Baucha akikabidhi mfano wa funguo kwa mshindi wa gari, Zubeda Abdalla Ali (kushoto) mkazi wa Donge, Zanzibar baada ya kushinda gari maarufu Kama KIRIKUU kwenye promosheni ya Ni Hero Yako iliyoisha hivi karibuni.
Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohamed Khamis Baucha (kushoto) akiongea wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi wa Promosheni ya Ni Jero Yako Tu jana. Kulia ni Rukia Mtingwa, Meneja Mawasiliano wa Zantel Tanzania.

Washindi wa gari, pikipiki na baiskeli kwenye picha ya pamoja.

Na Mwandishi Wetu.

Kampuni ya mawasiliano ya Zantel imekabidhi zawadi ya magari 2, pikipiki 5, baiskeli 8 na simu 2 kwa washindi wa promosheni iliyomalizika karibuni iitwayo ‘Ni Jero Yako tu’ ambayo iliwapa nafasi wateja wake wa Zanzibar nafasi ya kujishindia magari, pikipiki, baiskeli,fedha taslimu na simu za kisasa za interneti ya 4G.

Promosheni ya ‘Ni Jero Yako tu’ ya kampuni ya Zantel ,imefanyika kwa kipindi cha miezi mitatu kwa lengo la kuwashukuru wateja wake kwa kuendelea kuiunga mkono hususani katika kipindi ambacho ilikuwa katika mchakato wa kuimarisha miundombinu yake ya mawasiliano na wateja walishiriki promosheni hii kwa kununua vocha ya muda wa maongezi ya shilingi 500/-.

Hadi kufikia mwisho wa promosheni hii ambayo ilianza mapema mwaka huu, ikiwa imewalenga wateja wa Zanzibar, wateja 3 wameweza kushinda magari kwa kila mmoja aina ya Suzuki Carry, maarufu kama KIRIKUU, wateja 5 wamejishindia pikipiki kila mmoja, wateja 40 walijishindia baiskeli, wateja 90 kila mmoja alijishindia fedha taslimu shilingi 50,000/-na wateja 90 walijishindia simu za mkononi za kisasa.

Akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi iliyofanyika katika ofisi za Zantel za Zanzibar, Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohammed Khamis Mussa (Baucha) alisema,”Tunawashukuru wateja wetu kwa kuendelea kutuamini na kutuunga mkono, ndio sababu mwaka huu tuliwaletea promosheni ya kuwawezesha kujishindia zawadi zinazoweza kubadilisha Maisha yao kwa namna moja ama nyingine.”

“Zawadi tulizowapatia washindi wetu wa leo zinaweza kuwasaidia kujiongezea pato la familia, hizi Kirikuu pamoja na pikipiki wanaweza kuzitumia kufanya biashara ya usafiri na kujiongezea kipato na ndio maana tumekuja na promosheni zenye kutoa zawadi zinazolenga kuwanufaisha wateja wetu kiuchumi.”

Akizungumza baada ya kukabidhiwa zawadi ya gari Bi Fatma Mohammed Haji mkazi wa Magomeni Unguja alishukuru kampuni ya Zantel kwa kubuni promosheni zinazolenga kuwasaidia wateja wake hasa Zanzibar kumzawadia gari baada ya kushiriki kwenye promosheni ya Ni Jero Yako, aliongeza kuwa anatarajia kutumia gari hiyo kufanyia biashara ya kusafirisha mizigo.

“Nawasihi wateja wengine wa Zantel waendelee kushiriki kwenye promosheni mbali mbali za Zantel sababu promosheni hizi ni za kweli na wao wanaweza kuibuka washindi kama mimi,” alisema.

Hadi kufikia mwisho wa promosheni hii, wateja 235 wa Zantel walifanikiwa kujishindia zawadi mbalimbali na waliokabidhiwa zawadi jana ndio walikuwa wanahitimisha promosheni ya ‘Ni Jero Yako Tu’.

Wakati huohuo, kampuni ya Zantel inaendelea na promosheni inayojulikana kama “Tunaliamsha Kivingine” ambayo imezinduliwa hivi karibumi baada ya kampuni kuboresha miundombinu yake ya mawasiliano. Kupitia promosheni hii, wateja wa Zantel wamewezeshwa kufurahia huduma za internet yenye kasi kubwa kwa gharama nafuu kabisa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: