Mabondia Saidi Mpoma 'Kidedea' kushoto akitunishiana misuli na Vicent Mbilinyi baada ya kusaini mkataba wa kuzichapa Septemba 15, 2018 katika uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es Salaam. Picha na SUPER D BOXING NEWS.

Na Mwandishi Wetu.

BONDIA Vicent Mbilinyi amesaini mkataba wa kuzipiga na Saidi Mpoma 'Kidedea' Septemba 15 katika uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya kusaini mkataba huo, Mbilinyi amesema kuwa atafanya mazoezi ya kutosha ili aweze kushinda kwa kuwa ngumi kwake ni kazi kazi na kuwataka mashabiki wake wote kujitokeza siku hiyo kushudia mpambano uho kwani ato waangusha amejipanga vizuri.

Nae Saidi Kidedea amesema anashukuru kwa kupata mpambano uho kwana yeye siku zote achaguwi mabondia kwake yoyote anaekuja mbele yake kazi anayo na amepanga kummaliza mpinzani wake katika raundi za awali ili asiwachoshe mashabiki anao wategemea.

Aidha ameomba wapenzi wa mchezo wa masumbwi waje kumsapoti kwani ato wahangusha ata kidogo

Na mratibu wa mpambano huo, Rajabu Mhamila 'Super D' amesema siku hiyo kutakuwa na mapambano makubwa ambapo bondia Fred Sayuni atapambana na Haidari Mchango wakati George Dimoso atavaana na Abdallah Pazi 'Dulla Mbabe' na Imani Mapambano ataoneshana umwamba na Paul KamataSadiki Momba atavaana na Mohamed Kashinde na bondia machachari Tonny Rashidi atavaana na Said Zungu Ramadhani Shauri atakumbana na Saidi Amani.

Mbali na mipambano hiyo ya ngumi siku hiyo pia kutakuwa na burudani mbali mbali za muziki.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: