Mkuu Wa wilaya ya Arumeru Mh.Jerry Muro amewataka madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Arusha Dc kubuni vyanzo vipya vya mapato ili kuongeza kiwango cha ukusanyaji katika halmashauri hiyo.

Dc Muro ameyasema hayo hii leo katika baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Arusha ambapo amesema kuwa vipo vyanzo vingi vya mapato ambayo halmashauri hiyo inaweza kukusanya na kufika kiasi cha shilingi billion kumi.

Licha ya kutoa agizo hilo akalazimik kutoa tahadhari ya kutolipwa posho pamoja na kuvunjwa kwa baraza la madiwani kutokana na wao kushindwa kukusanya mapato

Mara baada ya kutoa agizo kwa baraza hilo La madiwani mwenyekiti wa halmashauri hiyo ndugu Noah Lembris amemsisitizia Mkuu wa Wilaya kuwa watazidi kufuata sheria zaidi ili kufikia maendeleo ya wananchi pamoja.

Katika kikao hicho cha baraza la madiwani kimejadili pia changamoto mbalimbali ikiwemo miradi ya maji iliyokwama kwa muda mrefu ambapo mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Dr Wilson Charles Mahera akasema ipo baadhi ya miradi iliyokamilika na inatarajiwa kuzinduliwa na mbio za mwenge wa Uhuru Katika Wilaya ya Arumeru
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: