Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla anatarajiwa kuhamishiwa katika Taasisi ya Mifupa (MoI) pindi atakapokamilisha matibabu yake katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alikolazwa tangu mwishoni mwa wiki.

Jana akijibu swali la mwandishi wa habari aliyetaka kujua maendeleo ya waziri huyo aliyepata ajali ya gari wiki iliyopita akiwa katika ziara ya kikazi, Mkurugenzi Mtendaji wa Moi, Dk Respicious Boniface alisema kuwa waziri huyo atahamishiwa kwenye taasisi hiyo wakati wowote. Alisema lengo la kumhamishia kwenye taasisi hiyo ni kuendelea na matibabu ya viungo vilivyovunjika.

Dk Boniface alikuwa akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu programu inayoendeshwa na taasisi hiyo ya uchunguzi wa umri kwa wachezaji wa timu ya taifa ya vijana walio chini ya miaka 17 ambao watashiriki michuano ya Cecafa itakayoanza jijini mwishoni mwa wiki.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: