Gari la Mbunge wa CHADEMA Lucy Magereri lenye namba za usajili T 348 CSR limepata ajali eneo la Issuna wilaya ya Ikungi mkoani Singida ambapo Dereva aliyefahamika kwa jina la Thomas Maro amepoteza maisha papo hapo.

Ajali hiyo imetoka leo Agosti 9 ambapo ndani ya gari hiyo alikuwepo dereva mwenyewe kwani alikuwa analitoa gari hilo Dodoma kulipeleka Shinyanga ndipo lilipogongana na Fuso lililokuwa linatoka Singida kwenda Dar es Salaam.

Dereva wa Fuso amepata majeraha madogo madogo huku mwili wa marehemu ukihifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa Singida.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Sweetbert Njewike amesema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa Fuso kuendesha gari upande ambao sio wake, na sasa amekamatwa yupo kituo cha Polisi kwa ajili ya mahojiano.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: