Mtanzania Victoria Mwanziva anaeendelea na masomo nchini China alipata fursa ya kushiriki Mkutano Maalumu wa Silk Road and Young Dreams, ulioandaliwa na Silk Road Cities Alliance (SRCA) na Beijing Belt & Road Cooperative Community (BRCC), pamoja na Renmin University. August 11-14, 2018 Katika Jiji la Beijing nchini China.

Mkutano huo ulikuwa na adhma ya kufanya tathmini ya Miaka Mitano kwa kuanzishwa kwa Belt and Road Initiative ya China na ulitoa wasaa wa Vijana kuwasilisha maoni yao juu ya Maendeleo ndani ya Belt and Road.

Victoria alipata wasaa wa kufanya presentation kuhusiana na Belt and Road na manufaa yake kwa Vijana wa Kiafrika na kushinda TUZO ya kuwa na moja ya Presentation bora zilizofanyika katika mkutano huo.

Mkutano huo ulileta pamoja zaidi ya vijana 100 kutoka katika nchi 26 shiriki za Belt and Road ikiwemo nchi ya Tanzania.

Tuzo hii ni ishara ya uwakilishi mzuri na heshima ya nchi ya Tanzania na Africa kwa ujumla.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: