Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mnacho iliyopo katika Kijiji cha Chimbila B, Kata ya Mnacho Wilayani Ruangwa, akiwa kwenye ziara yake ya kikazi ya siku nne, Agosti 9 2018 .
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akifurahia jambo na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mnacho iliyopo kwenye Kata ya Mnacho Wilayani Ruangwa, Agosti 9 2018. (Picha na Ofisi ya Naziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Kaimu Mkuu wa Shule Muhsin Ibrahim, baada ya kukagua darasa la kompyuta katika Shule ya Sekondari Mnacho iliyopo kwenye Kata ya Mnacho Wilayani Ruangwa Agosti 9 2018.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Chimbila B, kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Mnacho iliyopo kwenye Kata ya Mnacho, Agosti 9 2018. (Picha na Ofisi ya Naziri Mkuu).

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetenga sh. milioni 250 kwa ajili ya usambazaji wa huduma ya maji safi katika kijiji cha Chimbila ‘B’ kichopo kata ya Mnacho.

Ameyasema hayo leo (Alhamisi, Agosti 9, 2018) wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Mnacho wilayani Ruangwa akiwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kikazi wilayani hapa.Waziri Mkuu amesemaSerikali imedhamiria kumaliza tatizo la maji, ambapo itahakikisha wananchi wanapata huduma hiyo katika umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yao.

Amesema mbali ya maji kusambazwa kwa wananchi, pia yatasambazwa kwenye taasisi zote za umma zikiwemo shule za msingi na sekondari pamoja na vituo vya kutolea huduma za afya.

Awali, Waziri Mkuu alitembelea shule ya Sekondari ya Mnacho na kuzungumza na wanafunzi, ambapo amesema Serikali inatarajia kujenga mabweni mawili katika shule hiyo ili wanafunzi waweze kuishi shuleni na kupata fursa nzuri ya kujisomea.Waziri Mkuu ameyasema hayo baada ya wanafunzi wa kike shuleni hapo kuiomba Serikali iwajengee mabweni ili waweze kuishi shuleni na kupata muda mwingi wa kujisomea.

Wanafunzi hao wamemueleza Waziri Mkuu kwamba kitendo cha kuishi nyumba kinawakosesha muda wa kujisomea kwa sababu ya hupangiwa kazi nyingi wanapofika nyumbani, hivyo kukosa muda wa kujisomea.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, AGOSTI 9, 2018.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: