Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James akiwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Profesa Raphael Chibunda wapili kutoka (kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa NDC Profesa Damian Gabagambi wakwanza (kulia), Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo wapili kutoka (kulia), akikata utepe kuzindua Matrekta 10 ambayo ameyakabidhi kwa Chuo hicho cha SUA kutekeleza ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa wakati alipotembelea chuo hicho mkoani Morogoro tarehe 7 Mei 2018.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James akiangalia ubora wa moja ya matrekta hayo 10 aliyoyakabidhi kwa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine SUA.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James akizungumza katika hafla hiyo fupi ya kukabidhi ya matrekta 10 aliyoyakabidhi kwa Chuo cha Kilimo cha Sokoine SUA katika kiwanda cha kuunganisha Matrekta cha URSUS- TAMCO Kibaha mkoani Pwani.
Sehemu ya Matrekta 10 yaliyokabidhiwa leo kwa Chuo cha SUA ikiwa ni utekelezwaji wa ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa wakati alipotembelea chuo hicho mkoani Morogoro tarehe 7 Mei 2018.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: