Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe Stanislaus Mabula anaanzisha tuzo maalumu ya wanawake mahususi kutunuku wajasirimali na wawekezaji wanawake, ili kuenzi jitihada na harakati za kufikia uchumi wa viwanda kwa mstakabali wa ujenzi wa Maendeleo Nyamagana na taifa kwa ujumla

Haya yamebainishwa na katibu wa taasisi ya First community organization Florah Magabe akimwakilisha Mgeni Rasmi, Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe Stanislaus Mabula katika kongamano maalumu la uchumi, uwekezaji na mahusiano lililoitwa Red and Silver Party JB Belmond Hotel. 

Magabe alitumia adhara hiyo kutoa salamu za Mhe Stanislaus Mabula kwa kupongeza kikundi cha 'Mwanamke Mpambanaji' Kwa harakati zake za ujenzi wa fikra mpya za kiuchumi, kupitia kongamano lenye dhima ya kuwatoka wanawake na Vijana na wana Mwanza katika fikra za uchuuzi na kwenda katika ujasirimali na uwekezaji ili kufikishwa adhima ya uchumi wa viwanda.

Alifafanua kuwa Mbunge Jimbo la Nyamagana anatambua jitahada kubwa za wanawake katika kufikia uchumi viwanda Nyamagana kupitia harakati za elimu ya ujasirimali ili kutoka dhana ya kichuuzi, kufikia ujasirimali na uwekezaji. 

Mhe Mabula katika kwenda sambamba na dhima ya serikali ya CCM inayoogozwa na Mhe Dkt John Pombe Magufuli ya uchumi wa viwanda, amedhamiria kuanzisha Tuzo maalumu ya kutunuku wanawake kila mwaka, Kutoa mafunzo ya ujasirimali, uandikaji miradi na mpango wa Biashara na masoko kwa ushirikiano na taasis ya First community ili kutambua na kuenzi mchango, jitihada na harakati za wanawake katika kukuza pato lao, halmshauri na taifa ili kufikia uchumi wa Kati ambao ni wa viwanda.

Naye katibu wa Mbunge Jimbo la Nyamagana Heri Nkoromo Kipara amesema ofisi ya Mbunge imewezesha kusaidia usajiri wa vikundi katika halmashauri ya Jiji la Mwanza vipatavyo 375. Amepongeza kikundi cha Mwanamke Mpambanaji kujisajairi. Kadharika Ndg Heri amefafanua kuwa katika tengo la fedha 10% ya halmshauri Jiji la Mwanza 80% wanawake wameonesha nidhamu ya jedwari la marejesho na fedha hiyo kufanya Kazi iliyokusudiwa. Hivyo wanawake ninguzo kubwa katika ujenzi wa pato la taifa. Hivyo ofisi ya Mbunge itakuwa tayari kushirikiana na vikundi vyote vilivyosajiriwa halmashauri ili viweze kunufaika na tengo la 10% ambalo ni halali kwa Vijana na wanawake.

Naye Irene Mbowe mwezeshaji wa kitaifa na kimataifa alitumia jukwaa hilo kuhasa jamii ya kitanzania kufuata maadili na utamaduni za kiafrika kwa wanawake kutokebehi Maumbile ya wanaume kwakudhiki kupitia taswira matunda au mboga. Amewaasa wanawake kusimama katika nafasi ya utu wema, upendo, nidhamu na heshima kwa familia zao sanjali na kujihusisha na shughuli za ujasirimali na uwekezaji ili kujitegemea na kuondokana na dhana ya utegemezi.

Naye Mwenyekiti wa kikundi cha 'Mwanamke Mpambanaji' Paulina Francis alimshukuru Mhe Mabula kwa utayari wa kuwa mgeni rasmi sanjari kuwa mstari wa mbele kuunga jitihada za ukombozi wa wanawake kiuchumi ili kuwa nguzo katika ujenzi wa pato la wanawake na taifa. Kogamano hilo lilipambwa na wasanii wa kizazi kipya, wakufunzi wa Biashara na uchumi, pychologist, mahusiano pamoja na chakula cha Usiku.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: