Baadhi ya Vituo vya Usajili vinavyokamilishwa kila kila wilaya ya Unguja na Pemba 
Mifumo mipya iliyofungwa ili kuhifadhi kumbukumbu kisasa (kidigitali).
Baadhi ya Vifaa vilivyoko ndani ya vituo vipya.
Baadhi ya Vifaa vilivyoko ndani ya vituo vipya .
Jengo jipya ambapo Ofisi kuu ya Wakala wa usajili wa matukio ya Kijamii Zanzibar 
Mambo Msiige jengo la mwanzo lililotunza kumbukumbu za Wazanzibar za maswala ya matukio ya kijamii 
Zaharan Nassor Mhifadhi Mkuu wa Nyaraka wa wakala wa usajili wa matukio ya kijamii Zanzibar akionyesha Nyaraka Kongwe zaidi yenye majina ya Uzazi kuanzia mwaka 1909 hadi 1911 
Mhifadhi akichambua Taarifa katika Ghala la Nyaraka Ofisi kuu ya Mamlaka ya Usajili matukio ya kijamii Zanzibar. 
Dr Hussein Khamis Shaaban, Mkurugenzi mtendandaji wa wakala wa usajili wa matukio ya kijamii akikagua Nyaraka za Kale za vizazi na vifo ambazo zinachakatwa kuwekwa katika mfumo wa Kidigitali
Nyaraka zenye kumbu kumbu za wazanzibari za Uzazi, Vifo, Talaka, Ndoa na na utambulisho tangu 1909
Msajili wa vizazi na vifo Wilaya ya Kati Mkoa wa kusini Unguja akichambua Taarifa za mwananchi ili kujaza vyeti mbali mbali vya Wazanzibar 

*Serikali yajenga vituo vya kidigitali kila wilaya kutambua wakaazi wake

Na Mwandishi Wetu.

MWENDO ni wa kidigitali! Hivyo ndivyo unaweza kuelezea baada ya Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar kuamua kuingia kwenye mfumo wa kieletroniki katika kusajili wakaazi wa Zanzibar (E-ID CARD).

Hivyo Wakala hiyo imeamua kuingia katika mfumo wa kisasa zaidi katikka kuhifadhi kumbukumbu za wakaazi wa Zanzibar na kwamba hivi sasa taarifa zao muhimu zitatuzwa kwenye mfumo wa kidigitali.

Hayo yameleezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii, Dk. Hussein Khamis Shaaban wakati anazungumzia mikakati yao katika kuboresha na kuhifadhi taarifa za wakaazi wa Zanzibar ambapo ametumia nafasi hiyo kuwahamisisha kujitokeza katika kuboresha taarifa zao kupitia mfumo wa kidigitali.

"Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar imeamua kuanzisha vituo maalumu ambavyo vitatumika kuwasajili wananchi katika mfumo huo wa kieletroniki ambao maarufu zaidi kama mfumo wa kidigitali,"amefafanua Dk.Shaaban.

Pia amesema pamoja na kuhakikisha taarifa hizo zinakuwa katika mfumo wa kisasa wa kutunza kumbukumbu za wananchi wa Zanzibar bado wanaamini utasaidia katika kulinda usalama wa nchi sambamba na kuwatambua kwa kina Wazanzibari wenye makazi ya kudumu visiwani humo na kwamba mfumo huo unaifanya nchi hiyo kupiga hatua zaidi katika matumizi ya kieletroniki katika kutunza kutunza na kutambua watu wake.

Mfumo huu mpya utasaidia katika kutoa huduma kwa haraka kwani taarifa zitakazoifadhiwa katika mfumo huo zitatumika na mamlaka nyingine kama Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZRB), Idara ya Uhamiaji, National Internet Data Center (NIDC), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Msajili wa Makampuni, mfumo wa hosptali (e-health) na mfumo wa utalii.

Hata hivyo baada ya kukamilisha mifumo hiyo ya kieletroniki jukumu linaloendelea sasa ni kuhamasisha wananchi kuanza kujitokeza kwa ajili ya kuboresha kumbukumbu zao na siku za karibuni watatangaziwa siku ya kuanza kwa mchakato huo .

Aidha tayari kila wilaya kumejengwa kituo cha kidigitali ambapo vituo vyote katika wilaya 11 Unguja na Pemba vinaunganishwa na mkongo wa Taifa na Wananchi watajisajili huko huko wilayani na kuboresha taarifa zao, kwa sasa utaratibu wa kuchakata data za kale tangu daftari la mwanzo la mwaka 1909 zina hitahifadhiwa kidigitali katika kanzi data ya Taifa.

Kwa kukumbusha tu majukumu ya wakala hiyo ni kusajili matukio ya vizazi, vifo , ndoa , talaka na vitambulisho na kusisitizwa usajili huo unatakiwa ufanyike kwa njia ya kieletroniki na kubwa zaidi wakala imemua kuimarisha taarifa katika mfumo wake.

"Hivyo wakala inawatangazia Wazinzibar wakaazi wote kuwa itaendesha mchakato wa kuimarishaji taarifa kwa wote wenye vitambulisho vya Mzanzibar mkaazi pamoja na waombaji wapya katika mikoa yote ya unguja na pemba.

"Ratiba ya mchakato huu utatangazwa hivi karibuni na tunasisitiza kuwa uimarishaji wa taarifa za kila mmoja wetu ni wajibu wa kisheria na atakayeshindwa kuimarisha taarifa zake hataweza kukitumia kitambulisho chake katika huduma mbalimbali za kiserikali na za kijamii,"amesema Dk.Shaaban.

Amesisitiza wananchi wote waimairishe taarifa zao ili waweze kuvitumia vyema vitambulisho vyao vya Mzanzibari Mkaazi na kwamba "Kupitia mfumo huo, Wakala inatarajia kutoa kitambulisho kipya cha Mzanzibari Mkaazi cha kielektroniki (e-ID Card) na vyeti vya kuzaliwa vipya.

"Lengo kuu la mradi huu ni kuhakikisha tunaimarisha utoaji huduma za kijamii kwa Wazanzibari na wageni wakaazi wanaoingia na kuishi Zanzibar kwa madhumuni mbalimbali yakiwamo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii,” amesema Dk. Shaaban.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: