Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya akizungumza kwa mara ya kwanza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya Hai katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.
Baadhi ya Watumishi katika Halmashauri ya Hai wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa wilaya hiyo alipozungumza nao kwa mara ya kwanza.
Baadhi ya Madiwani wakiwa katika kikao cha kwanza na Mkuu wa wilaya ya Hai na watumishi wa Halmashauri hiyo.
Katibu Tawala wa wilaya ya Hai, Upendo Wela akizungumza katika kikao hicho.
Baaadhi ya watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai.
Baaadhi ya Wakuu wa Idara za Halmashauri hiyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai, Yohana Sintoo akizungumza katika kikao hicho.
Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,waichangia jambo katika kutano wa Mkuu wa wilaya ya Hai na Watumishi wa Halmashauri hiyo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Kanda ya Kaskazini.

MKUU mpya wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya amekemea vikali vitendo vya Rushwa vinavyofanywa na baadhi ya watumishi wa halmashauri ya wilaya hiyo hali iliyopelekea kutajwa kama mteja namba moja wa Taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa( TAKUKURU) katika mkoa wa Kilimanjaro.

Sabaya pia ameinyooshea kidole idara ya Ushirika katika Halmashauri hiyo ambayo inatajwa kushindwa kusimamia vyama vya ushirika hadi kupelekea kuingia mikataba aliyoitaja kuwa ya hovyo na yenye kujaa rushwa.

Katika kikao chake na watumishi wa Halmashauri ya wilaya kilicholenga kujitamburisha kwa watumishi hao Sabaya alisema Halmashauri hiyo inaongoza kwa ubadhilifu wa mali za umma na kwamba hadi sasa amepata taarifa za uwepo wa kesi nane zinazohusu rushwa.

“Mnaongoza kwa ubadhilifu na wa mali za umma,naambiwa kuna kesi nyingine zinaendelea na Takukuru inachunguza nyingine , hii ni aibu na ni fedheha kwa Halmashauri ,kama una mikono michafu hauna uhalali wa kumuubiri mtu habari njema niwaombe mbadilike”alisema Ole Sabaya.

Mkuu huyo wa wilaya alisema zipo taarifa ya kuwa katika Halmashauri hiyo kuna baadhi ya watu wamejijengea tabia ya kutaka kuonekana kama miungu watu kwa kufanya maamuzi bal ya kuwashirikisha watu wengine huku akimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo,Yohana Sintoo kulitazama hilo.

“Nimesikia wapo watu hapa, wao mnakaa kwenye CMT (kikaocha ushauri) mnafanya maamuzi yeye ni mungu mtu hapa ,ikifika wakati wa kutekeleza hawatekelezi ,mnawakatisha tamaa watumishi wengine walioko tayari kufany kazi ,walioko tayari kutekeleza yale tuliyoahidi wananchi tunategemea hao watu wabadilike”alisema Ole Sabaya.

“Kwa hiyo nategemea sana kwenye eneo la rushwa tuwe na mabadiliko makubwa ,lakini nikupongeze Mkurugenzi ,nilikuwa napitia taarifa ya CAG ya mwaka 2014 kwenda 2015 kulikuwa na hoja 83 leo amezishusha hadi kufikia hoja 6 jambo la kupongezwa lakini hata hizo sita ziondoke.”aliongeza Ole Sabaya.

Kuhusu Ushirika, Ole Sabaya alisema katika mambo ambayo Halmashauri hiyo imeanguka ni eneo la ushirika huku akiitaka idara ya ushirika kwa kushirikiana na ofisi ya Mwanasheria wa Halmashauri hiyo kupiia mikata iliyoingiwa kati ya Vyama vya Ushirika na wawekezaji.

“Kati ya sehemu tumefeli na tuna aibu kubwa ni eneo la Ushirika, kuna mikataba ya ajabu ajabu sijawahi kuona lakini mingine ni ninyi wenyewe mmeshindwa kutimiza wajibu wenu ,ukiangalia vile vyama vya ushirika na mikataba waliyoingia na wale wawekezaji na fedha wanazo zipata ,hata pengine kodi za serikali mmeikwepa kwa miaka mingi “alisema Ole Sabaya.

Alisema endapo Idara ya Ushirika ingetekeleza vyema wajibu wake leo hii kuisngekuwa kuwa na kilio cha mapato kwenye Halmashauri hiy kwani ingewawezesha kupata hata asilimia 2 kwenye mapato ya Vyama vya ushirika.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: