Kiongozi wa mradi, Caroline Ndosi akizungumza katika hafla hiyo ya uzinduzi.
Meneja wa Ushawishi wa Mradi huo, Gasirigwa Sengiyumva akielezea kwa nini ni muhimu kutoa elimu kwa umma kuhusu matumizi ya mitandao.
Mmoja wa viongozi (Project Leader) wa mradi huo Catherinerose Barreto akielezea umuhimu wa kushirikiana na wadau katika utekelezaji wa mradi huo.
Tulanana Bohela ni mmoja wa mameja wa mradi.
Asha Abinallah Mkufunzi wa Mafunzo yatakayoendeshwa katika huu mradi.
Wadau wakifuatilia mjadala wakati wa uzinduzi wa mradi huo.
Kiongozi wa mradi, Caroline Ndosi akijadiliana jambo na Tulanana Bohela ambaye ni mmoja wa mameja wa mradi.
Joshua Mwangasa kutoka Polisi Kitengo cha Makosa ya Mtandao (Kulia) ambaye alikua mwalikwa katika hafla hiyo ya Uzinduzi akiwa na Gasirigwa Sengiyumva wa Women at Web.
Wadau wakijadilia jambo mara baada ya uzinduzi.

Na Mwandishi Wetu.

Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Women at Web Tanzania imezindua mradi maalumu wenye lengo la kutoa mafunzo ya matumizi ya mitandao ili kuongeza uwepo wa kundi hili mitandaoni.

Mradi huo unaofadhiliwa na Shirika la DW Akademie la nchini Ujerumani una lengo la kuhamasisha matumizi bora ya mitandao ikiwamo kuongeza mijadala ya maendeleo kwa wanawake katika mitandao.

Akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi huo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam, mmoja wa viongozi wa mradi huo Caroline Ndosi amesema kwamba moja ya shughuli zitakazofanyika katika uhamasishaji huo ni mafunzo kwa wanawake yanayohusu njia za kujilinda na vurugu za mitandao, kutambua fursa zilizopo mitandaoni pamoja na mambo mengine.

Alisema kuwa kwa sasa Tanzania hakuna takwimu zilizo wazi za udhalilishaji wa wanawake kwenye mitandao japokuwa wengi waliopo wameshakutana na aina ya udhalilishaji kwenye mitandao, hasa ya kijamii.

“Idadi ya watu wanaomiliki smart phone inaongezeka hivyo kuongeza hatari za wanawake kuwa wahanga wa unyanyasi katika platform hizo, kwa hiyo kupitia mradi huu, pamoja na kuhamasisha wanawake kuongezeka kutumia hii mitandao, tutawapatia mafunzo ya namna ya kujilinda ama kutambua wale wanataka kuwafanyia ukatili.

“Lengo letu ni kuhakikisha kuwa kwa kuwa bado tuna ‘gap’ kubwa sana la wanawake kushiriki katika mijadala ya maendeleo nje ya mitandao, basi watumie fursa za mitandao kushiriki mijadala hiyo na kujiletea maendeleo,” alisema Ndosi.

Kwa kuanzia, mradi huo utaendesha mafunzo katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na pia kwa upande wa Zanzibar.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: